Kufeli kwenye maisha haina maana kwamba huwezi, au kufeli mtihani haimanishi kwamba umefeli maisha jifunze kutokukata tamaa.
Watu wengi wameshindwa kwenye maisha sio kwasababu hawawezi au sio kwa sababu wamefeli katika mambo mbalimbali ya kimaisha ila nikwasababu ya kukata tamaa
Mpendwa hata Yesu katika safari ya ukombozi alipokuwa ameubeba msalaba,Biblia inasema alianguka mara tatu na kila mala aliinuka na kuubeba msalaba wake na kuendelea mbele
Mpendwa inawezekana umekata tamaa lakini kumbe muujiza wako ulikuwa umekalibia kabisa, kwanini unakata tamaa mapema kiasi hicho?
Ninamjua kijana mmoja aliyefeli form IV na kupata ziro, akarudia mala ya pili akapata ziro na mala ya tatu akapata ziro lakini mala ya nne katoka na Division one
Fikiri kama angekata tamaa ingekuwaje, watu wengi tunakwama hapa tunakata tamaa mapema ni kweli unaumia vumilia songa mbele muujiza wako ukaribu
Mungu wangu akubariki sana kama umepokea kitu na unaamini comment ” kuanzia leo sitakata tamaa tena hata iweje lazima nifike kanani yangu katika jina la Yesu”
Kisha Fanyika baraka kwa wengine kwa kushare ujumbe huu na Mungu atakubariki sana sana
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.