Katika maisha watu waliofanikiwa walijifunza kutokuogopa jambo lolote linalosimama mbele yao kuwazuia kufika kwenye ndoto zao
Na watu wengi tumeshindwa kufika kwenye ndoto zetu kwasababu ya hofu inayoinuka ndani yetu yenye lengo la kutufanya tushindwe
Ninajua unayomalengo mazuri,unayo mawazo mazuri ambayo ukiyafanyia kazi yatakusaidia kimaisha lakini shida yako ni roho ya hofu
Biblia inasema kwenye kitabu cha
Yeremia 1:8
Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe,asema Bwana.
Bwana anasema unapoianza wiki hii usiogope kwa sababu ya hao Mungu yupo upande wako akuokoe lazima hiyo mipango yako itimie
Mazingira yasikuogopeshe, wewe Fanya,wewe anza na ninasikia kukwambia kuwa unaweza hata Kama woote waliokuzunguka wamekwambia huwezi Bwana anasema unaweza
Mungu akubariki ninakuombea katika wiki hii ukamuone Mungu katika kila eneo la maisha yako na Mungu akakusaidie uishinde roho ya hofu inayokukwamisha kuyafikia malengo yako
Uwe na wiki ya baraka katika jina la Yesu.na usiogope tena kwasababu ya hao Bwana yupo pamoja na wewe akuokoe.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.