Kuna kipindi unaweza kukipitia kwenye maisha haya,kikawa ni kipindi cha machozi na kilio na hasara katika kipindi maisha yanaweza kukosa maana kabisa
Nikiwa katika kuomba Bwana akaniambia wambie hata kama wamelia Bwana atawafuta machozi, walioona njaa na kiu hawata ona njaa na kiu tena
Ufunuo 7:16:17
Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.
Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.
Mpendwa wangu acha Mungu akufute machozi yako, aziondoe na hasara saa imefika hutalia tena ukiwa na uharibifu havitatajwa tena kwenye maisha yako
Ninakuombea neema ikufunike na Mungu akufute machozi uliyolia kwa muda mrefu Mungu akupe kicheko katika jina la Yesu
Ikiwa unaamini mwambie Mungu “Baba yatosha nifute machozi sasa na ukanipe kicheko katika jina la Yesu”
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.