Katika maisha ya kila siku tunazungukwa na watu wasiotamani kuona ukiongezeka katika eneo lolote kimaisha
Iwe ni kiuchumi, kielimu,kibiashara,kihuduma na nyanja zote za kimaisha. Lazima ufahamu kuwa unaishi na watu wa aina hiyo
Wapo ambao Mungu atakupa kuwajua na wapo ambao hutawajua. Na wakati mwingine hawa watu watakuchimbia mashimo
Nikiwa katika maombi Leo nimekuombea mashimo waliyokuchimbia ili usiolewe,ili usijenge,ili usinunue kiwanja,ili usisome, ili usipandishwe cheo
Nimekuombea katika hayo mashimo wakatumbukie wenyewe, Na hayo mabaya waliyoyakusudia juu yako yakawarudie wao katika jina la Yesu
Mithali 26:27 Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe;Naye abingirishaye jiwe litamrudia.
Nimekuombea siku ya leo kwamba acha Bwana akuinue mbele ya woote waliokuchimbia mashimo katika jina la Yesu
Katika mwaka huu acha Bwana akakupandishe cheo mbele ya wale waliokunenea mbaya kwa boss wako
Nimekuombea mwaka huu acha biashara yako ikachanue machoni pa woote waliokuchimbia mashimo ili kuiuwa biashara yako
Acha mwaka huu ikajulikane yakwamba humchi Mungu bure, humtafuti Mungu bure na acha ijulikane yakwamba Mungu wako ni mkuu kuliko Mungu wao
Na woote waliokuchimbia mashimo ninaona wakimtafuta na kumwabudu Mungu wako katika jina la Yesu
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.