Siku ya leo nasikia kuwatia moyo na kuwaombea watu ambao wanasikia kukata tamaa, watu ambao wamefika mahali maisha yao yamepoteza radha
Watu ambao ndoa,kazi, na kila kitu hakina maana, watu ambao wamezungukwa na uvuli wa mauti
Biblia inasema,,,,
Waamuzi 6:23 BWANA akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa.
Bwana ameniinua katika wakati huu kukutia moyo na kukuombea na kukwambia Amani ya Bwana iwe pamoja nawe
Biashara yako haitakufa,ndoa yako haitakufa,hutafukuzwa kazi, huo ugonjwa hautakuuwa, kwenye hiyo kesi Mungu atakutetea
Hayo mahusiano hayatakufa kama yale wala hutaachwa tena, huduma yako haitakufa, kampuni yako haitakufa sijui Mungu anaongea na nani
Nimekuombea kwa jina la Bwana wa majeshi wewe uliyekata tamaa na kuona uvuli wa mauti mbele yako, pokea amani na nguvu mpya hutakufa
Nimekuombea Mungu akupe tumaini jipya na kukufuta machozi na akayaimarishe magoti yako yaliyolegea katika jina la Yesu
Nimekuombea kuanzia leo maisha yako yakawe na maana tena, ndoa yako ikawe na maana tena, hutazarauliwa na kukataliwa tena pokea amani na kibali
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.