Wambie wasikate tamaa nipo pamoja nao katika mazingira yote wanayoyapitia sijawaacha
Na Bwana akaniambia wambie katikati ya upinzani na vita nitawalinda hawatadhurika hata watakapojikwaa hawatadhurika maana nipo pamoja nao
Ndipo nikasikia ndani yangu msukumo wa kusema na wewe najua kuna mahali unapita, na ninajua umeomba lakini hakuna kinachobadilika na wakati mwingine unapozidi kuomba ndipo vita inaomgezeka
Unisikilize mtu wa Mungu Bwana ameniinua Katika majira haya kusema nawewe kwamba hajakuacha,wanadamu wanaweza kukuacha lakini Bwana hawezi kukuacha kamwe
Ndipo Bwana akanipa mstari huu akaniambia wape na wausome kwa imani!!!!!!!!!!!!
Mwanzo 28:15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
Ninakuombea kila uendapo ukaone ulinzi wa Damu ya Yesu, iwe ni kazini, kwenye biashara, kwenye masomo, kila mahali Bwana akakulinde na kukuepusha na mabaya yote
Na katika mwaka huu uliokubalika nimekuombea Bwana akakutimizie yote aliyokuambia kuwa atafanya katika jina la Yesu
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.