Unapodhani au kuamini kuwa huwezi kufanya jambo fulani basi mfumo wako wa mwili wako kibaiolojia huanza kudhihirisha kile unachodhani hukiwezi
Kamwe huwezi kufanya kile unachofikiri huwezi kufanya
🔘Siri ya mafanikio ni kuamini kuwa unaweza na mwisho utaweza kulifanya jambo hilo.wengi hawafanikiwi sio kwasababu hawawezi kufanya mambo ya mafanikio
Bali ni kwasababu ya hofu iliyojaa ndani yao kuwa wataanguka,punde tu wakianza safari
🔘Kudondoka katika maisha haina maana kuwa umeshindwa kile ulichokianza,bali ni hatua moja wapo ya kufika pale unapopataka
Nguvu ya uthubutu ndio ngao imara dhidi ya hofu iliyotawala moyoni mwako
🔘Na ukiweza kuijenga nguvu hii ndani yako amini kuwa utaona matokeo mazuri sana na pengine utajilaumu kwanini hukuanza mapema kufanya
Nakutia moyo amini kuwa wewe ni bora sana na unaweza kuganya kile unachofikiria kama tu utaweza kupambana na tatizo ambalo hata hujui nini unachokiogopa
🔘Ondoa mawazo ya kufeli jiamini kuwa wewe umezaliwa kufaulu na hakika utafaulu kwani siku zote nguvu ya kutenda hujengwa na imani uliyoitengeneza.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.