Maadui wako hawajui una Mungu mtetezi.

Kati ya vitu ambavyo maadui zako hawajui nikwamba unae Mungu asiyelala, unaye Mungu anaekuwazia mema

Na pia hawajui ukuu na uaminifu wa Mungu uliyenaye,ndio maana ni rahisi kwao kukucheka na kuona Kama vile maisha yako yamefika mwisho

Mika 7:8 Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu.

Ninakuombea kama Bwana aishivyo hata Kama ulikuwa umeanguka na maadui zako wakafurahi kwamba tumemuweza,kwamba habari zako hazitasikika tena,nimekuombea ukainuke tena

Ninakuombea hata kama ulikuwa gizani Bwana akawe nuru kwako ili maadui zako wapate kujua kuwa unae Mungu asiyelala Kama mungu wao.

Nami nimekuombea ukainuke tena kiuchumi,milango yako ikafunguke na mahali penye giza nuru ikatokee katika jina la Yesu

Na kila utakalo lishika na kulifanya siku ya leo likafanikiwe katika jina la Yesu na nuru ya Bwana ikakuzukie Never Give up kesho yako ni nzuri kuliko leo yako


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment