Ni bora ufe ukijaribu kuliko kukata tamaa katika ndoto zako,mara ngapi umekuwa ukikata tamaa katika maisha yako?
Ni vitu vingapi umevikatia tamaa kuvifanya? Kwasababu tu ya magumu unayoyapitia au unayokutana nayo katika maisha yako
Acha nikwambie siku zote hakuna kitu kisicho na changamoto,mitihani,vikwazo na matatitizo mbalimbali, hasa unapokaribia mafanikio ndo unakata tamaa
Nasikia kukwambia upo karibu na mafanikio yako kuliko unavyofikiri usikate tamaaa woote unaowaona wamefanikiwa wamepitia magumu ila hawakukata tamaa
Fahamu kuwa unapolikaribia lango lako la muujiza vita huongezeka na majaribu huongezeka unapoona hayo ujue kuwa umekaribia jipe moyo usikate tamaa
Nimekuombea siku ya leo Neema ya kusonga mbele bila kukata tamaa iwe juu yako katika jina la Yesu
Acha ndoto zako zikatimie katika jina la Yesu hakuna kukata tamaa mpaka samweli wako azaliwe, watie moyo watu wawili watatu kwa kushare ujumbe huu na Mungu atakubariki
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.