Ee Israeli, asema hivi, Usiogope

Isaya 43:1:2Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.

Nimekuombea siku ya leo wewe unaepita katika mateso ya magonjwa, madeni, kukosa kazi na misiba ya kila aina sawa sawa na neno la Bwana hiyo mito haitakugharikisha

Nimekuombea siku ya leo najua unapita katika moto na umefika mahali huoni kama kunakutoka tena,huoni Kama kuna tumaini tena

Nimekuombea katikati ya huo moto hautateketea maana Bwana yuko upande wako hatakuacha uangamie

Acha Mungu ninaemtumikie akakuvushe hapo na kukutetea, acha Mungu ninaemtumikia akarudishe tumaini tena ndani yako katika jina la Yesu


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment