Jenerali Mwalimu Mchungaji Peter Mitimingi Ameaga dunia usiku kuamkia leo Mei 4 2020

Mimi Generali Cantona Joseph,nimepokea habari za kufariki dunia kwa, Mchungaji Mwalimu Peter Mitimingi kwa masikitiko makubwa sana.Nilifahamiana naye, mwaka 2006 akisoma nchini Kenya mahala nilikua nafanya kazi kipindi hicho kwenye chuo Cha biblia ICM hapa ndipo tulitangamana naye sana.Alipenda kusikiliza vipindi vyangu Radioni.Kwa.matani Unajua una sauti nzuri,ukiwa kwenye mwengoya.Kipindi hicho nilikua mhariri wa habari na msomaji habari Imani Radio Kitale, alikipenda Kiswahili changu,usemi wangu wenye mnato,lafudha iliyo bora ya kiswahili na ustadi wa kufikisha ujumbe nikitumia Lugha ya Kiswahili nikiwa Radio Imani.Tukajenga uhusiano wa mwana na mlezi.Siku zote alikua mwenye busara.Nimepokea habari za kifo chake, kwa masikitiko makubwa habari za kutuaga gafla kipindi hiki.Mwalimu Mchungaji Peter Mitimingi.Hili limenikosesha hamu.Alipenda kuniletea Kanda za nyimbo Injili nzuri kutoka Tanzania.Mwalimu uliwajenga wengi kwenye msingi wa dini,kupenda elimu ya injili na hili likakupa kiu kusoma na kufunzu na Shahada katika maswala ya elimu ya dini na Biblia. (Bachalors of Arts in Bible and Theology)hapo kwenye chuo nilicho hudumu Icm Kenya. Katika Theologia ya ICM,Kitale.Ulikua mtu wa kuigwa Generali Mitimingi. Mafunzo yako na kauli yako yenye hekima. Mume wa Mtu mwachie Mkewe usijifanye Fundi.Nitazikosa kauli hizi sana,ndoto yako ili itimie haianzi na mtu mwingine inaanza na wewe mwenyewe… Mwanaume mchakarikaji huwa hachagui kazi.Haijalishi ana elimu ipi.


Kuna tofauti Kati ya mke na mwanamke na mume na mwanaume wengine ni pasua kichwa walioletwa na upepo kuja kupasua kichwa chako. Nakumbuka ukinishauri unatumiaje leo yako,usipoitumia vizuri kesho utakuja juta. Utakapo ingia kwenye mahusiano kuwa makini na mwanamke ambaye utamchumbia, mwanamke asipo kutii kwenye uchumba hawezi kuheshimu katika ndoa.

Ukasema jitume kakangu, ukiona Kijana miaka 28- 30 anaishi kwa kutegemea wazazi wake,huyo si mume ni bomu kimbia.Kipindi hiki cha korona ulipenda kusema Imani ni nzuri pia hekima ni nzuri.Kwa Imani tuombe tutashinda na hekima nzuri tufuate magizo.

Generali,mpambanaji mbona kuondoka pasipo kwaheri Lala salama Generali.Makiwa kwa Jamii na huduma ya Voice of hope Ministries.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment