Ni maombi yangu usikiapo ingiza kwenye matendo ili unufaike na haya maarifa ;maana imani ispokuwa na matendo imekufa nafsini mwake.
Jambo la kwanza.
∆MAWAZO MABAYA YANAYOTOKA MOYONI MWAKO NA UKAYATEKELEZA.
Moyo wa mtu ni kama udongo na neno ni kama mbegu kufuatana na Marko 4:15″ hawa ndio walio kando ya njia LIPANDWAPO NENO;nao wakiisha kusikia huja Shetani, akaliondoa lile neno LILILOPANDWA MIOYONI MWAO.”nilichotaka uone hapo moyo ni kama udongo unaopandwa mbengu ambayo ni neno la Mungu(soma Marko 4:3-9); sasa ukisoma mathayo 13:24-25″ Akawatolea mfano mwingine , akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda MBEGU njema katika konde lake;13Lakini watu walipo lala , akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.”; Tunaona hapo mbengu njema ikipandwa (kama ipo mbegu njema basi ipo mbegu ambayo si njema)zote hizo zinapandwa ndani ya moyo wa MTU(hii mbaya inapandwa wakati gani , check watu walipo LALA, ulalaji unaongelewa hapa si wa mwilini ndio maana Yesu akasema kesheni basi ninyi kila wakati, sababu ukilala tu rohoni shetani anapanda mbegu ile isiyo njema moyoni mwako, sasa angalia mathayo 15:19″ Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya , uuaji, uzinzi, uasherati ;wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano” Tunajuaje kwamba hiyo ni mbegu iliyopandwa na hayo ndiyo matunda yake?
Ni rahisi tu Isaya 55:8-11……Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu ;HALITANIRUDIA BURE , BALI LITATIMIZA MAPENZI YANGU…., ” Sasa kumbuka tulikotoka kuwa neno ni mbegu , hapa Mungu anasema halita mrudia bure hadi litimize mapenzi yake , sasa kumbuka na yule anaepanda mbegu mbaya (Nimesema kama ipo iliyo njema basi ipo iliyo mbaya)’magugu’ kumbuka nae huyo mpandaji (adui shetani) hataki hiyo mbegu yake imrudie bure hadi itimize mapenzi yake shetani tunajuaje ? Check uzinzi , uasherati, uuaji, matukano, n.k sasa kama hujajua namna ya kujiombea ipasavyo ni rahisi hayo kukuharibia maisha yako .Yakobo 1:21″ kwahiyo wekeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio , na kupokea kwa upole NEN O LILE LILILOPANDWA NDANI, LIWEZALO KUZIOKOA ROHO ZENU ” check kama hili neno likipandwa ndani linaweza kuokoa roho zetu basi lipo litakalopandwa na likauwa roho zenu kabisa , check tena yakobo 1:22″ lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, …”ona hapo ile mbegu mbaya ikipandwa na kuzaa matunda ambayo ni mawazo mabaya shetani anaweka roho zake(mapepo kusimamia utendwaji wa neno lake )unakuta wazo la kuzini likija unahimizwa sana kutenda hapo ndo unaangamiza roho yako tayari lakini yakobo anasema tuwe watendaji wa neno anataka nini tukitenda tu tumeokolewa.1yohana 1:2″ Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile ROHO yako ifanikiwavyo .Sasa kufanikiwa katika Mungu huwa kunaanza rohoni kunatokelezea hadi mwilini , hapo ni rahisi kuelewa likipandwa neno baya na likazaa.
Mungu akutunze daima kama unasumbuliwa na mawazo mabaya.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.

