Zaburi 23:4

Nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,Sitaogopa mabaya;Kwa maana Wewe upo pamoja nami,Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

Moja kati ya jambo unalohitaji kulijua ni hili kwamba nyakati ngumu unazozipitia kimaisha ziwe ni za kiuchumi,kiafya au kimahusiano huwa hazidumu katika maisha

Kumbuka, kama kuna usiku kuna mchana pia,kama kuna mwanzo kuna mwisho pia,hakuna lenye mwanzo ambalo halina mwisho

Ninajua mahali Dunia inapita matumaini ya wengi yamepotea,ndoto za wengi zinazimika kama mshumaa,mipango ya wengi inakufa mioyo ya wengi imeugua kwa hofu

Ninakutia moyo wewe unaesoma ujumbe huu, nyakati ngumu huwa hazidumu kwenye maisha hata huu wakati utapita pia Amini tu katika bonde la uvuli wa mauti sio mahali Pakukaa ni mahali tunapita tu

Ninakuombea siku ya leo Mungu ninaemtumikia akutetee na akutoe katika hilo bonde la uvuli wa mauti na ukamuone Bwana katika jina la Yesu


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment