Bwana Yesu Asifiwe
Nataka nikutie Moyo mpya Na nguvu mpya ili uweze kuendelea mbele kwa ushindi kabisa kwa Jina la Yesu
🔹Inawezekana ulifika mahali ukakata tamaa kwasababu tu ulizungukwa na watu wanaokukatisha tamaa na kukuona hufai wala huwezi chochote
🔷 Inawezekana Umelia sana kwenye maisha yako kwasababu ya maumivu na majeraha ya moyo yaliyosababishwa na watu wako wa karibu tena uliowaamini na kuwategemea
🔹 Yeremia 31:3:4
BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
👉👉Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi.
🔹Hata kama umechekwa na kuumizwa na kuachwa, Bwana amenituma nikwambie iko mala ya pili waliokucheka na kukuumiza hawakujua kwamba iko mara ya pili
🔹Huhitaji Kulia wala kukata tamaa iko mara ya pili Mungu atakujenga tena na utajengeka, Mungu atakupamba tena nawe utapambika
🔹Waliozoea kukuona katika michezo ya wanao ila watashaa kukuona katika michezo yao wanaofurahi wakikuuliza wambie huu ni upako wa mara ya pili
🙏 Mimi na mke wangu tumekuombea yule Mungu aliyetutoa jalalani mahali pasipo na tumaini na kutupa upako wa mara ya pili akakuonekanie na wewe
🙏Amini tu iko mara ya pili, Mungu atafanya.hii ni siri kubwa sana unahitaji kuijua acha wakucheke leo,acha wakuzarau leo ila iko mara ya pili Mungu atakupamba na kukupa kicheko tena
Kama unaamini comment
“Bwana yatosha nipe upako wa mala ya pili nitoe katika michezo yao wanaolia, nipe kutokea katika michezo yao wanaofurahi”
Na itakuwa,fanyika baraka na kwa wengine kwa kushare ujumbe huu na Mungu atakubariki sana tunakuombea na tunakupenda sana
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.