Luka 23:34 Yesu akasema, Baba, uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
Niliposoma nakutafakari mstari huo nielewa mambo mengi
1. Lengo la hao maadui waliomsurubisha Yesu ili kuwa ni kumuuwa na kummaliza kabisa
2. Kwa kutokujua walifikiri wakisha muuwa pale msalabani ndo wamemaliza na walijua ndo wamefuta jina lake kabisa duniani
3. Walijua njia moja wapo ya kummaliza ni kumuuwa tena kifo cha aibu
Lakini kuna kitu Yesu alikuwa anakijua ambacho wao walikuwa hawakijui
Luka 18:33
nao watampiga mijeledi,kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.
Laiti kama wangejua kuwa huyu wanaemuuwa leo siku ya tatu atafufuka na nguvu nyingi na utukufu mwingi wasingefanya yoote waliyoyafanya
Ndio maana Yesu aliomba Mungu awasamee maana hawajui walichokifanya kina madhara gani kwao na kina faida gani kwa Yesu na kwa kanisa
Najua kabisa hata wewe
1. Umezungukwa pande zote na maadui wanaotamani kuila nyama yako
2. Maadui ni wengi wanaotamani kukumaliza na kufuta ukumbusho wako kabisa duniani
3. Maadui ni wengi wanaosubiri kuaibika na kuanguka kwako
4. Maadui ni wengi wanaokusemea maneno ya uongo ofisini kwako, kwenye ndoa n.k
Laiti wangejua wanachofanya nikukupandisha wewe wasingethubutu kufanya kabisaaa
Maana kupiga teke chura ni kumuongezea mwendo!!!!!!!!!!!!!!!
Nimekuombea katika msimu huu wa pasaka Bwana akakuinue na kukuheshimisha katika ya maadui zako waliosubiri kuanguka kwako
Nimekuombea maadui zako waliokupiga teke wakijua wamekumaliza wakajua hutainuka tena, wakaone ukianza kwa mwendo mpya katika jina la Yesu
Nimekuombea kila walichofikili wamekiuwa na kukizika kwenye maisha yako iwe—–
● Ndoa yako
● Afya yako
● Kibali chako
kazini na cha
biashara
● Vyeti vyako
● Biashara yako
Nimekuombea siku ya tatu vikafufuke pamoja na Kristo kwa utukufu mkubwa kwa namna ambavyo watakapoona wafedheheka na wajute kwanini tulimfanyia hivi?
Nimekuombea usilie tena wala usiwaogope hao maadui zako wanaokutendea mabaya kuna kitu hawajakijua ndio maana wanakutendea ubaya
Wambie maadui zako kwa kukomenti “kuna siku ya tatu hata nikianguka Kuna kusimama tena hata nikiwa Gizani Bwana ni nuru yangu” na itakuwa katika jina la Yesu
Uwe na pasaka njema na Bwana akakufanyie kicheko katikati ya maadui zako. Watumie na wengine ujumbe huu ikiwa unaona utawafaa na wao
Wako shambani mwa
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.