Yesu Kristo apewe sifa!
Ninawasalimu kwa Jina la Yesu Kristo!
Wateule,
✒ Usiku wa Leo nikiwa kwenye maombi nimesikia sauti ikiniambia jipe moyo mkuu hata hili litapita,
✒ Nikasikia sauti ikiniambia mtie moyo huyo :-
– mwenye shida kwenye
ndoa
– mwenye matatizo ya
kiafya
– mwenye kesi
mahakamani
– aliyezulumiwa haki
yake
– aliyesingiziwa mambo
ya ajabu
– aliyeachwa na watu
wake wa karibu
-pito lolote
✒Mpendwa jipe moyo mkuu hata hilo litapita , kama Mungu alivyokuwa mwaminifu katika lile hata hili ni mwaminifu
Isaya 41: 10-13
anasema,
Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.
Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.
Katika Hii mistari kuna mambo kadhaa ya kujifunza;
1. Kama huyu mtu anaambiwa usiogope Mimi nipo pamoja nawe,
✒ Inamaanisha alifika mahali akaona Kama uwepo wa Mungu haupo kwenye maisha yake kulingana na mahali anapopita.
✒Nami najua kabisa unapitia mambo magumu mno lakini nasikia kukwambia usiogope hata kama ni jambo gumu kiasi gani amini kuwa Mungu anapita na wewe hapo.
✒Wanadamu wanaweza kukuacha lakini Mungu hawezi hata kwenye moto atapita na wewe.
2. Kama anamwambia usifadhaike, Mimi ni Mungu wako
✒Ina maanisha kuwa mambo magumu aliyokuwa anayapitia huyu mtu yalimfadhaisha
Neno kufadhaika
_ni kama vile kukosa nguvu za kuendelea, kuchoka, kukosa tena nguvu za kuomba maana umechoka ni kama vile unaona Mungu kanyamanza.
Nami usiku wa Leo nikasikia sauti Kama sauti ya maji mengi ikiniambia mwambie -:
– Huyo mama aendelee
mbele Mimi ni
Mungu wake
– Huyo kijana aedelee
mbele Mimi ni
Mungu wake
Kwa nini Mungu anamwambia aliefadhaika kuwa Mimi ni Mungu wako?
✒ Alikuwa anatafuta kurudisha imani ndani ya huyu mtu iliyopotea kutokana na anakopita ambako kumempelekea kufadhaika na kushindwa kuendelea tena
✒Mungu anajaribu kumwambia Mimi Mungu ulieamua kuniamini ni mwaminifu na sio kwamba sioni ninaona magumu unayoyapitia
Na ndio maana chini anaanza kumhakikishia kuwa kwasababu Mimi ni Mungu wako -:
1. Anamwambia naam nitakutia nguvu
– kwa nini anaanza na jambo hilo kwa sababu anajua umechoka umeishiwa nguvu za kuendelea mbele hata waliokuzunguka kwa kiswahili cha mjini wanajua umeishiwa.
✒Ninakuombea asubuhi ya leo Mungu akutie nguvu Kama unaamini haijalishi wapi unapita au jambo gani unalipitia comment ” Hata hili litapita Yesu nitie nguvu nivuke hapa salama”
Kisha hubiri pamoja nami kwa kushare ujumbe huu na Mungu atakubariki sana
Amen!
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.