Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi.

“Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Haya! Kwea wewe, ukamwinulie Bwana madhabahu penye kiwanja cha Arauna, Myebusi. Basi Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi, kama Bwana alivyomuamuru… Naye Daudi akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za Amani. Basi Bwana aliiridhia nchi, na tauti ikazuiliwa katika Israel” (2Sam.24:18, 25).

Mungu aliiadhibu Israel kwa ugonjwa wa tauni. Watu 70,000 wakafa kwa wakati mmoja(2Sam.24:15). Lakini Mungu alighairi adhabu ya kuwauwa watu waliokuwepo Yerusalem(2Sam.24:16). Nabii Gadi akamwambia mfalme Daudi akamjengee Mungu madhabahu katika kiwanja cha Arauna Myebusi(2Sam.24:18). Mfalme Daudi alitii na kufanya hivyo. Mara baada ya kujenga madhabahu hiyo, tauni ikakoma katika Israel (2Sam.24:25).

Kiwanja cha Arauna ndipo ambako mfalme Sulemani alimjengea Bwana Hekalu (2Nya.3:1).Hapa ndio mlima Moria, ambako Ibrahim alimtoa sadaka mwanawe Isaka(Mwa. 22:2).Lakini Badala ya Isaka kutolewa sadaka, Mungu akampa Ibrahim mwana kondoo wa sadaka, Isaka akapona kifo(Mwa.22:12,13). Yesu Kristo alisulubiwa Golgotha (Mk.15:22). Huu ni mlima uliopo mahali ambapo ni moja ya vilima vya milima ya Moria. Kwa hiyo madhabahu ya Arauna ina uhusiano na madhabahu ya Golgotha.

Naye Rais wa Tanzania,ameona jinsi COVId-19 inavyoangamiza dunia(Dan mpaka Beer-sheba). Hivyo ameitikia wito wa kujenga madhabahu ya maombi ili Mungu aiponye Tanzania (Yerusalem). Wito mkuu wa maombi hayo. Kenya piai hayo maombi,Kuomba Mungu kwa ajili ya KUIPONYA Nchi yetu ili TUSIANGAMIZWE. Kwa hiyo, tuombee mambo yafuatayo:

FortuneBaraka Photography

SHUKURANI

  1. Mshukuru Mungu kuwa kama ilivyokuwa kwa Daudi, Rais Uhuru Kenya na John Magufuli kutii sauti ya Mungu ya kujenga madhabahu ya maombi Nchi nzima.
  2. Mshukuru Mungu kwamba kama ilivyokuwa kwa Yerusalem, ndivyo itakavyokuwa kwa kwa Kenya na Tanzania.Tauni itakoma wakati huu ambako Rais pamoja na watu wake wanajenga madhabahu ya maombi katika nchi.
  3. Mshukuru Mungu kwamba Kanisa limekubali kusimama mahali palipobomoka (Eze.22:30).
    TOBA
  4. Fanya toba Binafsi ili Mungu asikie na kukubali maombi yako(Neh.1:5-11)
  5. Fanya toba ya kimaombezi kama Musa, kwa ajili ya nchi ya Kenya na Tanzania. Soma kwa sauti (Kut.32:11-14).
  6. Msihi Mungu kwa Damu ya Yesu ya Agano Jipya iliyomwagika katika madhabahu ya Golgotha arehemu Tanzania na watu wake. Soma kwa sauti (Zab. 32)
  7. Tubu kwa ajili ya wanaodhihaki wito wa Rais Magufuli wa kufanya maombi ya kitaifa na kuona kuwa maombi hayo si msaada. Soma kwa sauti (Ezr.9:6,7)
    MAOMBI
  8. Omba Mungu aondoe COVID-19 katika nchi ya Kenya na Tanzania kama alivyofanya kwa mji wa Yerusalem. Hata kama COVID-19 imeua watu katika nchi nyingine isiwe hivyo hapa kwetu (2Sam.24:16).
  9. Omba Mungu aangalie kifo cha mwanawe Golgotha na atuondolee Janga la COVID-19 (Rum.8:32).
  10. Omba sadaka ya Yetu pale Golgotha ikafidie ugonjwa wa COVID-19 badala ya vifo vya watu kama ilivyokuwa kwa Isaka na mwana kondoo(Ebra.9:14) (Mt.20:28).
  11. Kataa nguvu za kaburi na roho ya mauti kwa wagonjwa wa COVID-19. Soma kwa sauti (Hosea.13:14) na (1Kor.15:55-57).
  12. Omba ulinzi kwa wasiougua na omba kwamba ugonjwa usiendelee kusambaa kwa watu wengine. Soma kwa sauti (Zab 91).
  13. Futa maneno yaliyosemwa na watu kuwa Afrika itashuhudia maiti zikizagaa mitaani kwa sababu ya COVID-19. Tuma malaika mharibu akaue maneno hayo katika ulimwengu wa roho (Isa.54:16, 17).
  14. Endelea kuombea watalaam wa afya. Maji na Damu ya Yesu viwafunike, viwakinge na kuwatakasa na maambukizi ya virusi vya Corona(Yn.19:33)
    MWISHO
  15. Mshukuru Mungu kwa maombi yote uliyofanya, ukiamini kuwa atajibu.
  16. Muombe Mungu ashughulike na mahitaji yako binafsi. Atakabali sadaka yako hii ya maombi(Zab.20:1-4)
    AMINA.
FortuneBaraka photography

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment