Kongowea mswahili,Ni jina alituzwa baada ya kushinda tuzo shuleni katika simulizi ya Siku njema.Maelezo ya mwanzo mwandishi anatumia kwenye maelezo Msanifu Kombo, katika kitabu siku njema,Kongowea anazaliwa katika familia na anamfahamu Mama yake Zainabu makame,mwimbaji wa Taarabu,maeneo ya Tanga Tanzania, anakejeliwa na watoto wengine mwanaharamu,Kongowea anapitia changamoto ya familia baada mama yake, mzazi kufariki,Maisha magumu inchini Tanzania, alihifadhiwa na shangazi yake alipotuzwa kuwa mtunzi bora hadithi aliyoandika anapokezwa Jina Kongowea mswahili,jina lake la kuzaliwa Ni Msanifu Kombo.

Changamoto pale kwa shangazi yake wivu na mahangaiko yanapelekea kuanza safari yenye kiza kingi kutafuta aliko baba yake,alimtazama kwenye picha tuu,Mama yake hakumweleza mengi.Lakini alipotaka kukata roho,anamwelezea kwa kusitasita mwanangu ba,,ba,,,ko akiwa hajamaliza kutamka mengi anakata roho. Amuj Isokum,ambaye Alikua ni mwandishi wa mashahiri tajika.Alikua amelibadili Jina lake Juma Mukosi.Ili likidhi uandishi wake wa tasnia ya uandishi.Kongowea anajipata Mombasa hali inakua ya kijungu jiko, Mombasa anasukuma rukwama,anahangaika na maisha,hadi aliposafiri hadi Kitale.
Ni riwaya ya Siku njema ninayoichambua jinsi nilivyo ielewa maana nilitahiniwa riwaya hii kidato Cha nne.
Wengi ambao wamebahatika kusoma hiki kitabu wanauliza,ninafahamu Tanga Ipo pwani ya Tanzania,Mombasa Ipo pwani ya Kenya,Je Kitale Ipo,Suwerwa Ipo,Makutano kwa ngozi je Ipo?
Nachukua fursa hii kusema hivi ni swali nzuri.
Kitabu kabla kutamatika kinaelezea Kongowea mswahili akiandika safari yake ya Maisha chumbani,nyumba aliyo ridhi kutoka kwa Baba yake mzazi.anaendelea na kuandika,mke wake Vumilia Binti Abdala anamtazama mme wake amechoka anampiga pambaja anamurahi akapumzike.Anachungulia dirishani na kuona mda umeenda Sana.
Jibu,Kitale Ni Mji upo katika kauti ya Transnzoia,tunakuza mahindi kwa wingi,Ni ghala la nafaka nchini Kenya, Cherangany Ni eneo bunge letu na Suwerwa Ni Kijiji jirani na Bwake na Makutano kwa ngozi.Hapo Ni kijijini kwetu upande wa pili Ni Kijiji Cha Bonde nyumbani kwao Mwenda zake Profesa Ken Walibora. Usanifu wangu wa kutema madini simulizi na andishi unatokana na hali ya kupenda kazi zake na kujifunza kutoka kwake hasa chachu ikiwa Ni mtu nimemjua hili lilinitia nguvu.Kuwa mwanahabari na mwandishi linajitokeza maana wanaonifahamu nilipenda kukichambua hiki kitabu.Ni kupitia uandishi wa mashahiri na makala ya kiswahili kwenye Taifa la leo/Jumapili nilichapishwa

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.