WANAOMWABUDU MUNGU KIUNABI MPO?YANI PROPHETIC WORSHIPER.

Nakusalimu mpendwa mwana wa Mungu ktk jina la Yesu.

Namheshimu sana mkristo anayejitambua.

Najua tunaishi kwenye nyakati ambazo watumishi wengi wanataka waonekane kuwa ni watumishi. Tena wanataka waonekane wao ni wa ‘level’ fulani!!

Mitume, Manabii, Wachungaji, Walimu, Wainjilisti wanataka kuonekana ktk level fulani.

Waimbaji wanataka waonekane wao ni wa level fulani. Kila mmoja akipata nafasi ya kutumika anataka ajionyeshe yeye ni bora kuliko wengine.

Mwabuduo hana sehemu ya kujionyesha. Yeye magotini na Mungu wake. Huna haja ya kujionyesha kuwa wewe ni muombaji ambaye Mungu anakusikia na kujibu. Huna haja ya kujionyesha kwamba Bwana amekupa access ya kujihudhurisha mbele za kiti cha enzi. Huna haja kabisa.

Kama unajitambua muombaji huu ndiyo wakati mzuri wa kuonyesha huduma yako mbele ya kiti cha enzi. Wakati dunia nzima inalia na #Covid-19, huu ndiyo wakati wa kujihudhulisha mbele za kiti cha enzi na hoja zenye nguvu kumsihi Mungu kwa mkono wake wa kuume wa uponyaji uponye dunia hii.

FortuneBaraka photography

“Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.

Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake”

Zaburi 46:1:3

Nakusihi ktk jina la Yesu ewe muombaji usitaharuki bali chukua hatua madhubuti kuifanya huduma hii pasipo hofu ktk kipindi hiki.

FortuneBaraka photography

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment