Neno lilipomjia Eliya katika mwaka wa tatu,akajionyeshe kwa Ahabu;Naye ataleta Mvua Juu ya nchi.

Biblia Takatifu. 1 Wafalme 18:1-2
[1]Ikawa baada ya siku nyingi, neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu, kusema, Enenda, ukajionyeshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi.
[2]Basi Eliya akaenda ili ajionyeshe kwa Ahabu. Na njaa ilikuwa nzito katika Samaria.
Wakati huu wana wa Mungu wanaitaji sana chakula cha kiroho,nawale wote waliozuiliwa kutoka majumbani mwao wanaitaji pia chakula cha roho.

Wakati wa nabii Elia ilikuwa shida sana ndani ya miaka mitatu kulikuwa na njaa kali sana,na iliwagusa kila mtu ata manabii pia ni km leo hali hii inamgusa kila mtu kwa namna fulani tuombe sana Mungu aweke wepesi.

FortuneBaraka Photography

Biblia Takatifu. 1 Wafalme 18:3
[3]Ahabu akamwita Obadia, aliyekuwa juu ya nyumba yake; (na huyu Obadia alikuwa mwenye kumcha BWANA sana;
Tunahitaji wakina Obadia watu waliowekwa kwaaji ya kuhifadhi wateule wa Bwana kwa namna yeyote kipindi hiki
Pamoja na mazingira magumu bado Obadia aliwahifadhi manabii wa Bwana Mungu wa Israel kwa kuwaficha mapangoni

Fortune Baraka Photography


Biblia Takatifu. 1 Wafalme 18:4
[4]kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
Usiogope na yaamini tuu maono yako japo tunapita kwenye wakati mzito lkn maono yapo pale pale
Neno ili liwe chakula kwako likupe nguvu nakuamini kila uliloomba litatimia tuu kwa wakati wa Bwana

FortuneBaraka Photography

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment