Yote yanawezekana ukiweza kuamini neno tuu.

Karibu katika Mafundisho ya Neno La Mungu Tunaenda Kukumbushana Nini maana ya wewe kuweza au uvuke katika Kipindi kigumu unatakiwa uamini Neno Inawezekana.

Tufunue Biblia Zetu kabla sijaendelea Mathayo;19;25
Marko:9;19-25:,Luka 18;27

UTANGULIZI
Katika Marko;9;19-25 Tunaona Ushuhuda wa kijana Aliyekuwa Anateseka na kifafa ukiziwi na ububu toka Mtoto Mzazi wake Anamweleza Yesu Kuwa Pepo Alijitaidi Kutaka Amuue Lakini Mungu alimlinda

Mzazi anaendelea kushuhudia Amezunguka huku na kule na pepo wa kifafa alikuwa akimwagusha kwenye Moto Sasa nyingine alimrusha na kumdodosha Mwanae wakati mwingine aliangukia maji ya Moto.

Mwili wake ulikuwa umejawa majereha
Yesu Akamuuliza Mzazi huyo; Je Unaami nikimuombea Atapona
Mzazi;Naamini
Yesu;Nakwambia Kwamba ukiweza Leo KUAMINI NENO Inawezekana kwa Mungu yasiyowezekana kwa wanadamu ujue mwanao atafunguliwa.
Mzazi;Naamini lakini Namuomba Mungu imani yangu Aifanye isiwe na Hofu juu ya Neno Inawezekana kwa Mungu.
Yesu alimuombea yule Mwanae akafunguliwa Kupitia Yule Mzazi KUAMINI NENO Inawezekana kwa Mungu licha ya kuwa alikuwa Amezunguka na Mwanae ameteseka nae muda mrefu lakini Kupitia KUAMINI NENO TU Inawezekana aliponywa Mwanae.

Tupo Katika vipindi vya watoto wote wa Madhabahu hii kila mwaka Tunatembea na Neno Kuazia mwaka huu 2020 uinjilisti wetu wa kwanza tuliufanya Nairobi kanisa la marafiki, Friends Church Headquarters Ngong road Nairobi.Huduma ya pili tukasafiri kauti ya Vihiga kanisa la Word of Faith Praise Centre Mbale.Huduma ya Fortune Int’l Ministries,yenye kauli mbiu Impacting a Godly Generation imebuniwa kuhimiza kizazi hiki,kuwafunza ukuu wa Mungu,kuwashauri kurejelea musingi wa kumwabudu Mungu maana Mungu yupo katikati ya sifa.

Bird wing Dove Logo Template vector illustration

2020 Ni mwaka wa Ushuhuda
Namshuhudia Mungu Anavyozidi Kutenda na Wanaofika Mikutano yetu ya uinjilisti inayoandaliwa na kundi la waimbaji wa nyimbo za injili Fortune Int’l Ministries watu wanafunguliwa na wegine Shuhuda wanazileta wapo watu wanafika walishakata Tamaa na matumaini wakija wanafunguliwa Kupitia Neno la Mungu tu wanakaa wanafundishwa na katika Masomo wanashuhudia wakiponywa wakibadilishwa wakiinuka Tena kupitia nyimbo za Sifa na maabudu.

YOTE YANAWEZEKANA KWA Mungu Ni wewe KUAMINI NENO walioamini Kicheko walicheka walio Amini Kibali walikiona wanaoamini Sasa hivi mwaka huu Ushuhuda lazima Neno likatimie kwao Sababu Nimeona nakushudia nguvu ya KUAMINI NENO.

Mwaka huu Ndio Tumepata mtikisiko wa Kidunia Corona imeinjia katika Neno lenye nguvu 2020 Ni mwaka wa Ushuhuda na Mungu Anaenda kuweka Ushuhuda Kupitia kunyamazisha kabisa uoga nà tishio la Corona.

HATUA ZINAZOKUPA USHINDI KATIKA KUAMINI NENO.
1:Unatakiwa Usome mstari wa Biblia au Uwe na mstari unaotembea nao.
Kisha chukua Neno TU si mstari wote.
Mfano huu Ndio mstari wako
Luka : Mlango 18

27 Akasema, Yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa Mungu

Unachukua Neno Yanawezekana kwa Mungu
Njisi utakavyoutumia Unasema Mimi Cantona nasema Haijalishi historia yangu ilikuwaje nimekuwa DHAIFU wa kuomba Sina kazi lakini mwenzi huu Inawezekana kwangu Kupata kazi kuimarika kiimani maana Luka:18;27 imesema Inawezekana Mungu kubadili historia yangu.

Sasa wewe weka mstari unasimama kwa Ajili ya wakati ulio nao

2:Simamia msimamo wa Neno usiyumbishwe Mara umesimama na Neno Hili Mara Lile

3:Jitie nguvu kuwa Kupitia Neno la Mungu unaloliamini linaenda kubadili maisha yako.

4;Usijiweke nyuma katika kuomba nakutumia Neno ulilonalo usiwe unakaa bila kuomba na usiwe mgumu wa kuokoka ili ulelewe kiroho ukue Kama upo busy Fatilia Masomo haya yanakuinjia kigajani mwako.

5:Utavuka Amini na shika Tu Ulichonacho Neno lako Ni Ushindi wako usiwe unaomba hauna Neno unalosimama nalo.

FortuneBaraka Photography

HASARA ZA MTU ASIYEAMINI NENO AU KUWA NENO NDANI YAKE.
1;Utakuwa unalibeba Andiko lote nzima hitaji moja una maneno mengi

Mfano Tuchukue mstari huu mtu anautumia kuutamka wote kumbe alitakiwa aangalie anahitaji ardhi au Kiwaja basi anaweza kwenda Kiwanja chochote ambapo anajua anaweza kupanunua anakanyaga nakusimama kisha anasema nyayo zangu zimekanyaga kiwanja hiki Naenda kupamiliki nakupashikilia Napanunua katika jina la Yesu sawa sawa na Yoshua;1;3 imesema Mimi Cantona kila ninapopakanyaga Mimi Ni Kwangu mwenye eneo hii auze nakuniuzia gharama nitakayo sababu nataka nimjegee Mungu Ushuhuda katika jina la Yesu.

Sio Unaanza umesema kila mahali zitakapokanyaga nyayo Zangu….hupaswi uwe na Maneno unatakiwa uwe na Neno

Yoshua:1;3
3 Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa

2:Utateswa na kuendeshwa na Falme za ngiza endapo huna Neno huamini

Hujawahi kuona mtu anafika kwa Mtumishi anamwambia umefunguliwa halafu Yeye analishika Neno tu anaponywa

3:Bila Kuamini NENO Ni Kama bengu uliyotupia kwenye jiwe kila siku unaimwagilia halafu unajipa matumaini utamea TU wapi mpaka uje uone umekufa.ndiye mtu anayependa tu Kuombewa Neno Hana ndani Yake

4:Huwa Mtu Anashika Mistari na maandiko mengi akijua kuwa na maandiko Shetani atamuongopa Shetani haongopi maandiko au wingi wa Mistari anaongopa Sana mtu mwenye Neno Ambalo limetoka katika mstari kwenye Biblia akachukua Kuamini Neno.

5:Huwa Ni mateso na mahagaiko mtu asiye na Neno.

FortuneBaraka Photography

Ninawaombea Mungu awape Neema Ya Roho wa Ufahamu awape kulielewa SoMo Hili ili mtoke katika mateso mbalimbali na fikira za Damu na nyama maana hupotosha nakumtesa Mtu lakini Roho Mtakatifu huweza Kujenga fikira na Ufahamu wenye nguvu Shetani hawezi kuwashinda ninyi mmeitwa katika Roho na Mungu akazidi kuwafungua wote mlipo Popote katika jina la Yesu.

Tupende Mafundisho ya Neno la Mungu na Tusimamie Neno la Mungu linasemaje na ufalme wa Majeshi na roho chafu tutazipinga katika jina la Yesu.

FortuneBaraka Photography

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment