Mwanajeshi anapokua vitani.

Mwanajeshi anapokuwa vitani anayaamini maji aliyo yabeba kwenye kibuyu chake na sio kunywa kunywa tu kila maji atakayo kutana nayo.Anaweza akakuta dimbwi la maji hata kama ana kiu hawezi kuyanywa kwakua anaweza kunywa kumbe adui anaye pigana nae amemuwekea sumu kwenye yale maji.Neno la Mungu ni maji ya uhai lkn sio kila neno ni neno la Mungu mengine ni makapi hufai kuyasikiliza na kuyatumia hufai kuyanywa,yawezekana umefikia hatua mbaya mpaka ya kushindwa kuwaamini watumishi wa Mungu kwasababu umekunywa maji machafu mengi yamekuharibu tumbo mpaka hauamini tena Maji yatokayo juu.Ili uweze kutambua neno la Mungu lzma uwe na Roho wa Mungu ili akusaidie kuelewa,Mungu leo akupe masikio ya Roho yako ikaelewe neno halisi la Mungu,na wala usifate fate tu kila unacho sikia ukizani ni neno la Mungu
Usiku wa leo nitafundisha namna ya kumsikiliza Mungu na neno lake jiunge nami ukipata kibali kupitia whatsapp group wengi wamefunguliwa kupitia hili na Mungu akubariki sana



Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment