Wewe ni chombo muhimu sana mbele za Bwana

Wakati uliokubalika ni sasa,huu ndio wakati wa kufanya mabadiliko kwenye maisha yako ukimuamini Mungu kwa kila hatua yako.
Unajua kuna neno linasema sisi tumeumbwa kwa kwa mfano wa Mungu,neno hili halimaanishi tunafanana sura au umbo na Mungu hapana Mungu ameweka mamlaka ndani yetu kama vile yeye alivyo na mamlaka ndio maana ninaombea wagonjwa mbalimbali wanapona hiyo sio nguvu yangu bali ni uweza wa Mungu uliopo ndani yangu,nina kemea mapepo yanakimbia kwakua mimi ni mfano wa Mungu.
Mimi na wewe tumeumbwa kwa mfano wake hata wewe una uweza na mamlaka ndani yako,jiamini alafu muamini Mungu aliye kuumba.Amini kwamba atakuvusha hapo ulipokwama wala ww sio wa kufeli hata kidogo,
Usivunjike moyo wewe ni chombo muhimu sana mbele za Bwana hata kama watu wanakuona si chochote lakini mbele za Bwana ww ni wa thamani Kubwa.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment