Mungu hakumzuia Farao kuwafwata wana wa Israel

Mungu hakumzuia Farao kuwafwata wana wa Israel walipotoka Misri tena aliufanya moyo wake kuwa mgumu kabisa ili asikate tamaa ya kuwafatilia lakini alikua na maana yake,alimpiga pigo ambalo mpaka leo ni historia aliangamiza majeshi yake na siraha na magari na farasi ndani ya bahari ya shamu,hata wewe ambaye unaona adui yako amekazana sana kukufatilia maisha yako kila ukiomba mashambulizi ndio yanazidi usiogope kama Musa alivyo waambia wana wa Israel hawa wa Misri mnaowaona leo hamtawaona tena ndivyo na mimi nakwambia hao adui unaowaona leo,hayo mateso unayopitia leo,hizo shida masengenyo na dharau unazo zipata leo hutazipata wala kuziona tena hili ni neno la Mungu linakuijia leo.Mungu anamfanya adui yako asikate tamaa ya kukufata ili aje mpige na kumuangamiza kabisa na watu wote watamsujudia Mungu wako.Hiyo ndiyo Tabia ya Mungu Usiogope

Watu wanakutazama na kukutathmini kulingana na wao walivyo, ndio maana si ajabu wakakuhusisha na mambo ya kushindwa sio kwa sababu umeshindwa ila ni kwa sababu hawajawahi kushinda na hawaamini kuna mtu anaweza kushinda.
Ila Mungu anakutazama vile ulivyo, ndio maana anataka ushinde zaidi ya vile unavyoamini una nguvu ya kushinda. MTAZAMO WA MUNGU KUHUSU WEWE NI KUKUPATIA AMANI NA ANAKUWAZIA MEMA. Acha kuumizwa na mtazamo wa watu juu yako.
WATU HUVIONA VITU SI KAMA VILIVYO BALI WAO WALIVYO.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment