Na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili (speaks better things than that of Abel)
Damu za hawa wawili zote zilimwagwa pasipo hatia, ILA MOJA ILINENA MEMA ZAIDI (better things) KULIKO INGINE Ambayo bila shaka ilinena mema (good things) ila sio mema kuliko (better things).
Nimewahi msikia mtumishi mmoja akisema damu ya Habili ilinena nanukuu ” Mungu! kaka yangu kaniua bila hatia naomba umsamehe hajui alitendalo” haya ni maneno mema.
Ila damu ya Yesu ilisema ” Baba Mimi nimebeba dhambi na uovu wao, nichinje Mimi ili wao wapone” hiki ndicho kinachoitwa (mema kuliko).
Tunapofikia hapo lazima tuelewe tunaye KUHANI BORA KULIKO KUHANI YEYOTE ALIYEWAHI KUTOKEA, JE! UKO TAYALI KUMPA MOYO WAKO ABEBE DHAMBI ZAKO?
KAMA UKO TAYALI OMBA MAOMBI HAYA!
Bwana Yesu karibu ndani yangu, nakupa moyo wangu, naomba uwe Bwana na mwokozi wa maisha yangu.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.