Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Imeandikwa katika Mithali 3:33 Kwamba “Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.”
Kumbe Uovu unaweza kuleta laana.
Usifarijiwe kwamba hakuna laana wakati matendo yako maovu yaliyo kinyume na utaratibu wa MUNGU, hayo matendo yanaweza kukuletea laana tena laana ya MUNGU mwenyewe.
✓Ndugu, ishi maisha matakatifu ya Wokovu yaliyo ya haki ili uepukane na laana.
✓Ndugu, timiza wajibu wako kwa MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi.
✓Ndugu, zingatia maagizo ya MUNGU ambayo usipoyazingatia yanaweza kukuletea laana ya MUNGU.
Hapa sizungumzii laana zisizo na sababu bali namzungumzia laana yenye sababu, laana ya MUNGU siku zote ni laana yenye sababu.
Hapa sizungumzii laana za wanadamu au laana za mawakala wa shetani, bali namzungumzia laana ya MUNGU.
Biblia inasema laana hiyo inaweza kuwapata waovu mbele za MUNGU.
Mithali 3:33 “Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.”
Inawezekana hujui laana ni nini.
✓Laana ya MUNGU ni nini?
Laana ya MUNGU ni ukosefu wa radhi za MUNGU katika jambo fulani.
✓Laana za kibinadamu ni nini?
Laana za kibinadamu ni apizo alitoalo mtu kwa mtu mwingine ili afikwe na mabaya?
✓Laana za kishetani ni nini?
Laana za kishetani ni apizo alitoalo wakala wa shetani kwa mtu fulani ili huyo mtu afikwe na mabaya?
Laana za kibinadamu kuzishinda ni rahisi sana maana zingine ni laana zisizo na sababu hivyo hata bila kufanya lolote hizo laana hazifanyi kazi.
Hata kama ni laana zenye sababu na zimekushikilia hakika basi anahitajika Mwenye nguvu kiroho kuliko mtoa laana hivyo ukimkimbilia YESU KRISTO hiyo laana haitabaki.
Kuzishinda laana za kishetani ni rahisi mno, ni wewe kumkimbilia Mwenye nguvu kuliko nguvu zote za giza, na huyo ni Bwana YESU KRISTO hivyo ukimkimbilia YESU KRISTO utakuwa umesababisha laana zisiwe na uhalali kwako.
Njia ya pili ya kuzishinda laana za kishetani ni kuombewa katika jina la YESU KRISTO, vifungo vya giza vikiondoka na hiyo laana imeondoka.
Sasa kama laana ameitoa MUNGU utafanyaje?
Hapa lazima mwili wako usisimke maana MUNGU ndiye Alpha na Omega, ndiye mwanzo na mwisho.
Sasa huyo Alpha na Omega ndio kakulaani kwa sababu ya uovu wako, utafanyaje ili laana ya MUNGU iondoke kwako?
Mambo ya kufanya.
- Tubu kwa MUNGU toba ya kweli.
- Hakikisha umempokea YESU KRISTO Kama Mwokozi wangu na yaache matendo yote ambayo husababisha laana.
- Timiza wajibu wako kwa MUNGU katika KRISTO YESU.
Ndugu, inawezekana watumishi wengi Sana wamekuaminisha kwamba hakuna laana, inawezekana wanakufariji ujinga kabisa wakati ukweli ni kwamba una laana ya MUNGU kwa sababu ya uovu wako.
Inawezekana wanakupoteza kabisa kwa maneno yao ya kukufariji kwamba hauna laana wakati maisha yako halisi unayajua wewe.
Katika mafundisho yangu Mimi Cantona Joseph huwa sipendi kamwe kuwazungumzia watumishi wengine, ila kwa kukutahadhalisha chunguza mwenyewe maandiko ili usije ukabaki katika laana huku ukijifariji kwamba hakuna laana.
Ndugu dawa ya laana ya MUNGU ni kutubu kwake na kuacha hicho kilichosababisha laana.
Asomaye na afahamu.
ROHO MTAKATIFU akusaidie kujua ukweli halisi.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.