Mungu atakupitisha kwenye njia ngumu na hatari wakati mwingine njia zenye majonzi na hofu njia ambazo mwanadamu wa kawaida hawezi jaribu kutamani kupita lkn mwisho wa hatari ni Amani isiyo na kifani,mwisho wa uwoga anakupa ujasiri utasahau majonzi atakupa furaha isiyo kuwa na kipimo hiyo ndiyo tabia ya Mungu.
Pale ambapo watu wamefikia mwisho kufikiri ndipo Mungu huanzia hapo.Unaezani kwamba umefikia ukomo Mungu ndio anataka kuanza hapo.Ni maombi yangu leo Mungu akakuinue na kukutoa hapo ulipo kwama na akuvushe kwa mkono wake wenye nguvu
Kila jambo na wakati wake,kila wakati una maana sana na kusudi lake.Kama ulikua unalia kuna furaha inakuja mbele yako,kama ulionewa na kudharauliwa heshima inakuja kwako,waliokupiga vita sana mwaka jana mwaka huu ni majira ya amani na furaha kwako.
(Mhubiri 3;1) Huu ni wakati uliokubalika na wote wenye imani watapokea miujiza mikubwa kwa Jina la Yesu.
Kilichofanya wakina Mariam na Magdalena kuendelea kwenda kaburini alipo lala Yesu baada ya kufa wakiwa na manukato na manemane na uvumba sio tu upendo bali walillishika neno kama alivyosema Yesu kabla ya kufa atasurubiwa na kufa lkn siku ya 3 atafufuka,kwaio walikua wanafanya hayo yote wakiamini atakuwa hai tena baada ya siku ya tatu.
Hata wewe kuwa na imani na neno la Mungu na kulishika,Yesu akasema ndugu zake ni wale wanaolishika neno la Mungu na kulitii.Mungu anakwenda kujibu maombi na hitaji lako kabla ya mwaka kuisha amini neno hili katika Jina la Yesu.
CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo…
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email:fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com
cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!
All Rights Reserved @2020/FortuneBarakaEntertainments.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.