Mkono wa Mungu Ni Msaada mkuu

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU.

Kuna utendaji wa aina nyingi wa mkono wa MUNGU.

Ayubu 27:11 “Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa MUNGU; Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha.”

Katika funuo zote ambazo mimi Cantona Joseph,nimewahi kufunuliwa sijawahi kuona msaada mkubwa kupita mkono wa MUNGU.
Sijawahi kupata ufunuo unaofanya kazi kama ufunuo wa mkono wa MUNGU.

Isaya 14:27 “Maana BWANA wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma?”

Katika maombi yako jifunze kumuomba MUNGU ili mkono wake ufanye kazi na utashangaa ushindi utakaoupata.

Mambo kadhaa kuhusu mkono wa MUNGU.

  1. Mkono wa MUNGU unaweza kukuokoa dhidi ya adui.

Mfao hai Ni huu.
Ezra 8:31 “Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; NA MKONO WA MUNGU ULIKUWA PAMOJA NASI, AKATUOKOA NA MKONO WA ADUI, NA MTU MWENYE KUTUVIZIA NJIANI.”

Ni muhimu kujua kwamba ukimtii MUNGU mkono wake utakuwa na wewe lakini ukimuasi MUNGU na mkono wake utakuwa kinyume na wewe na hataweza kufanikiwa kamwe.

  1. Inakupasa tu unyenyekee chini ya mkono wa MUNGU ili MUNGU akuinue katika baraka.

1 Petro 5:6-7 ” Basi NYENYEKEENI CHINI YA MKONO WA MUNGU ULIO HODARI, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”

  1. Hakuna mwanadamu au nguvu za giza wanayeweza kuugeuza mkono wa MUNGU ambao MUNGU ameuelekeza kutenda jambo.

Hesabu 11:23 “BWANA akamwambia Musa, Je! Mkono wa BWANA umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako, au sivyo.”

  1. Mkono wa MUNGU ni wenye uweza mkuu sana.

Yoshua 4:24 “watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa BWANA, ya kuwa ni mkono wenye uweza, ili wamche BWANA, Mungu wenu, milele.”

  1. Ukimsihi MUNGU ili mkono wake upeleke mapigo na uharibifu kwenye ngome za wakuu wa giza hakika hakuna atakayepona.

Mfano hai ni mkono wa MUNGU ulivyonyooshwa kwa Farao na Misri yake.
Kutoka 9:3 “tazama, mkono wa BWANA u juu ya wanyama wako wa mifugo walioko kondeni, juu ya farasi, na juu ya punda, na juu ya ngamia, na juu ya ng’ombe, na juu ya kondoo; kutakuwa na tauni nzito sana.”

Omba maombi ukimsihi MUNGU ili aunyooshe mkono wake wa kutoa mapigo, aunyooshe kwenye madhabahu za giza wanaokusumbua, aunyoshe kwa wachawi na majini wanaokusumbua na aunyooshe kwa kila mkuu wa giza na mkuu wa anga na wakala wa shetani yeyote ambaye amekufunga au kukuonea muda mrefu.
Katika maombi yako msihi MUNGU ukimuomba aunyooshe mkono wake wa kuachilia mapigo kwa nguvu za giza na mkono wa MUNGU utafanya kazi.
Hakikisha tu unamwambia MUNGU aunyooshe mkono wake wa kufanya nini.

Kumbu 2:15 “Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa kati ya marago, hata walipokoma.”

  1. Wanaomwasi MUNGU watakutana na mkono wa MUNGU wa kutenda mabaya.

Waamuzi 2:15 “Kila walikokwenda mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.”

  1. Unaweza ukashangaa mkono wa MUNGU ulivyofanya kazi siku zote ambazo Nabii Samweli alikuwa kiongozi Israeli.

1 Samweli 7:13 “Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli.”

  1. Dhambi zako zinaweza kuufanya mkono wa MUNGU usikuokoe.

Isaya 59:1-2 ” Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”

  1. Omba MUNGU akujulishe mkono wake.

Yeremia 16:21 “Basi, tazama, nitawajulisha, mara moja hii nitawajulisha, mkono wangu, na nguvu zangu; nao watajua ya kuwa, jina langu ni YEHOVA.”

Kwanini ni muhimu ufunuliwe juu ya mkono wa MUNGU?

Ni kwa sababu unaweza kujaribu kutengeneza sehemu ambapo MUNGU ameweka mkono wake ili pawe palivyo, hivyo utakuwa unafanya kazi bure kupatengeneza maana hapatatengenezeka.

Unaweza kuona adui zako wana nguvu kwa sababu mkono wa MUNGU haupo hapo, hivyo omba MUNGU akujulishe mkono wake na ukifunuliwa juu ya mkono wa MUNGU kukusaidia basi hata kama maadui zako ni taifa zima, uwe na hakika wewe utawashinda.

  1. Ijue kanuni ya ufanyaji kazi wa mkono wa MUNGU.

Mkono wa MUNGU unaweza kuwa juu ya mtu mwema ili kumtendea mema.
Lakini pia mkono wa MUNGU unaweza kuwa juu ya mtu mwovu ili kumtenda mabaya.

Ezra 8:22b ” …. Mkono wa MUNGU u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao.”

Hivyo mkono wa MUNGU unaweza kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja hivyo jifunze Neno la MUNGU sana ili uelewe utendaji kazi wa mkono wa MUNGU.

Nini ufanye katika maombi yako na maisha yako?

  1. Ishi maisha matakatifu katika KRISTO YESU ili uuruhusu mkono wa MUNGU wa kutenda mema utende kwako.

Matendo 4:29-31 ” Basi sasa, BWANA, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, UKINYOSHA MKONO WAKO KUPONYA; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu YESU. Hata walipokwisha kumwomba MUNGU, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa ROHO MTAKATIFU, wakanena neno la MUNGU kwa ujasiri.”

  1. Omba kwa MUNGU kwamba mkono wako uwe juu yako ili kukuokoa.

Ezra 8:31 “Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; NA MKONO WA MUNGU ULIKUWA PAMOJA NASI, AKATUOKOA NA MKONO WA ADUI, NA MTU MWENYE KUTUVIZIA NJIANI.”

  1. Nyenyekea chini ya mkono wa MUNGU ili akuokoe. 1 Petro 5:6-7 ” Basi NYENYEKEENI CHINI YA MKONO WA MUNGU ULIO HODARI, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”
  2. Msihi MUNGU ili mkono wa MUNGU upeleke mapigo kwa maadui zako katika ulimwengu wa roho wanaotoka kuzimu na wamekutesa muda mrefu.

Zaburi 21:8-9 ” Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. BWANA atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.”

Ndicho pia kilimpata Farao na Wamisri katika Kutoka 9:3

  1. Okoka na ishi maisha matakatifu daima ili mkono wa MUNGU wa kutenda mabaya usiwe juu yako ili kukutenda mabaya.

Waamuzi 2:15 “Kila walikokwenda mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana.”

  1. Msihi MUNGU kwamba mkono wake uwe daima juu ya adui zako ili kuwazuia kukudhuru kivyovyote.

1 Samweli 7:13 “Hivyo Wafilisti walishindwa, wasiingie tena ndani ya mipaka ya Israeli; na mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Wafilisti siku zote za Samweli.”

  1. Mshukuru MUNGU kwa ajili ya kazi ya mkono wake.

Zaburi 52:9 “Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha MUNGU wako.”

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

Bwana YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.

CantonaJoseph’s contacts

Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/

Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.

Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph

LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo

Management Fortune Baraka Entertainments

Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com

Email:fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com

cantona.online254@gmail.com

Contacts +254748836127

Wewe ni wa maana sana!

All Rights Reserved @2020/FortuneBarakaEntertainments.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment