1
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2
Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3
Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
5
Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
7
BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8
Njoni myatazame matendo ya BWANA, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
10
Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
11
BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
HAYA NI MANENO YANGU YA USHINDI NA MAOMBI YETU KWAKO ULIYEIONA SIKU YA LEO
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.