Soma Yakobo 1:13…
Mungu anaweza kuacha jaribu likupate lakini hawezi kusababisha na lazima ujue kuna utofaut kati ya kuacha na kusababisha
Fikiria mtoto akiondoka na kwenda kufanya uovu fulani halafu jambo baya likampata je atasema ni baba yake ndie aliyesababisha?
Unapokua Mkristo umeokoka lazima ujue kumtambua Mungu
Jaribu linapokupata ni Mungu ameliacha kwakua ameamini unaweza kulivuka
Na wala Mungu haachii jaribu linalokuzidi uwezo unapoona ni kubwa sana jua Mungu ameona unaliweza ndio maana ameliacha tu likupate
Na Mungu anafanya hivyo kwakua anataka ajitukuze kupitia wewe utakapo kimbia jaribu unamfanya Mungu ahuzunike ni sawa na kukimbia mtihani
Huwezi kuvuka kwenda daraja lingine kama unakimbia mitihani. Ukiona jaribu mbele yako ni wakati wa kushangilia utambue kumbe hata wewe Mungu anakuamini
Si ni wewe ambaye uwa unasisimka ukisikia habari za uwezo wa Mungu
Si ni wewe ambaye unakasirika sana ukisikia watu wanamsema vibaya Mungu wako
Onyesha upendo wako na ujasiri wako mbele ya matatizo na majaribu yako
Simama na umuoneshe Mungu kwamba unampenda na unamuelewa
Muoneshe Mungu kwamba unamuelewa na uko tayar kufanya yale atakayo kwambia
Unapolia na kukimbia jaribu ni kuonesha kwamba Mungu anakuonea
Ni kuonesha kwamba hauko tayari kuwaonesha watu kama una mpenda na kumuamini
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.