NAMNA YA KUOMBA MAOMBI YA KUMFICHUA ADUI YAKO

Watu wengi wanaomba lakini bila kujua adui yao ni nani
Lazima ujue adui yako ni nani na ana siraha gani na yuko wapi ili unapotupa makombola yampate sawasawa usipoteze muda kupigana bila kujua unampiga nani,na hii ni kanuni hata majeshi yanapo pigana lazima umtambue adui yako tofaut na hivyo mtapigana wenyewe kwa wenyewe na pia ujue adui yako anatumia siraha gan na yuko wapi.

Katika nakala iliyopita nilieleza kwamba shetani ni Roho na hawezi kufanya kazi zake bila kuingia ndani ya mwili.Adui yako ni mjanja sana na anakupiga kwa akili sana,ili kumtambua unahitaji Roho wa Mungu ili akusaidie wakati ule Sauli,Barnaba,na wakina Simioni walipokwenda kisiwa cha Pafo walikuta kuna mchawi mmoja anaitwa Elima.

Elima alikuwa akiaminika watu wakizani yeye ni mtu mzuri sana na walimyegemea lkn yeye alikua ameuteka moyo wa Liwali Sergio na kumuendesha kama anavyotaka (Matendo 13 anzia mstari wa 1 na kuendelea ili upate maana nzuri) watu wa kisiwa kile hawakujua kama Elima ni tatizo mpaka walipokuja watu wanaoongozwa na Roho ndipo wakaona.
Adui wa kisiwa kile ni yule mchawi Elima au Bar-yesu.

Kumjua adui yako ndiko kuna ushindi wako huwezi kuwa unaomba tu bila kujua unaomba nini na unapigana na nani

KANUNI ZA KUOMBA
1.Ukiwa unaomba usivute picha ya sanamu fulani au kitu fulani cha kutisha

2.Hakikisha umeomba maombi ya toba na umsihi Roho wa Mungu awe na wewe kwenye maombi yako.

3.Usiombe kwa kuhisi fulani ndio adui yako:shetani anaweza kukuletea picha kichwani ukazani ni kwel kumbe anakudanganya

4.Muombe Mungu moja kwa moja,Yesu alifundisha akisema mkiomba salini hivi Baba Yetu uliyembinguni.

Kwaio unapo omba omba moja kwa moja kwa baba aliye mbinguni usipitie kwa jina lingine tofauti

5.Baada ya hapo muambie Mungu akuoneshe adui yako,unapo omba mwambie Mungu unataka kumuona adui wa maisha yako kwakua neno linasema ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu,ufalme wake upo katika Roho na kila anaye zuia mafanikio na njia zako lzma aachie kwakua Mungu amekupa kumiliki na kutawala na tayari alisha kuahidi baraka na malango yako yawe wazi (Isaya 60;11….)

Adui yako anaweza kuwa anakufata kwa njia ya wanyama au sura fulan za watu huwajui wanakukimbiza au kukufanyia jambo fulani

6.Muambie Mungu afungue sura zao.Kama unaota paka,au wazee vikongwe,au watu warefu,au kundi la watu liko gizani ujue unayo nguvu ya kuwashinda adui zako kwaio wanajificha ili usiwaone na kuna wakati wanaweza kubadilika kuwa mbwa wakaanza kukukimbiza ndotoni ujue hao ni wachawi

7.Maombi haya yaombe usiku hasa wa manane utapata matokeo makubwa sana
Wakati mwingine nitafundisha siraha za Mungu ili uweze kuzitumia kuwashinda adui zako.Mungu akubariki


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment