VITU HALALI AU MATENDO HALALI YANAVYOTUKOSESHA FURSA KWA MUNGU.

Paulo anasema vitu vyote ni HALALI ila si vyote VIFAAVYO na vyote ni halali ila si vyote vijengavyo 1 kor 10: 23

Msitari huu nimeuelewa vizuri baada ya kisoma kisa cha Mfalme Daudi alipotaka kumjengea Mungu hekalu na Mungu akamkatalia kwa sababu mikono yake ilijaa damu. 1 Nyak 28:3 1 wafalme 8:19

Daudi alikuwa mtu wa vita na aliua wengi kihalali kabisa kulingana na kazi yake LAKINI PAMOJA NA UHALALI WA KAZI YAKE ALIKATALIWA KUFANYA JAMBO HILI TUKUFU LA KUJENGA HEKALU LA BWANA.

Unaweza kuwa una nafasi, cheo, kazi na ni halali kwako kufanya jambo lolote na ukawa halali kabisa kulingana na utaratibu, maelekezo, au hata sheria za nafasi hiyo. ILA NATAKA KUKUKUMBUSHA USIPOKUWA MAKINI UNAWEZA JIKUTA HUFAI KWA BAADHI YA KAZI AMBAZO UNAZIWAZA KUZIFANYA MOYONI UTAKAPOTOKA KWENYE NAFASI HIYO.

Daudi ilikuwa damu za watu alioua kihalali kabisa ( ukimuondoa Uria) SIJAJUA KWAKO SABABU YAWEZA KUWA IPI.

NI VYEMA UKAFANYA JAMBO HALALI NA LIFAALO KWA FAIDA YA VILE UNAVYOTAKA KUWA MBELENI.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment