Anasema yeye hakuomba kuwa maarufu, ila kile alichopewa kufanya kilimpa umaarufu, na KWA sababu ya umaarufu huo siku moja alishambuliwa na kuandikwa vibaya na gazeti, na kama ilivyo kawaida hakuweza kujitetea wala kusahihisha kuhusu tuhuma na kashfa waliyomwandika, MAANA WALIOMWANDIKA HAWAKUJALI USAHIHI WA VILE ALIVYO BALI WALIANDIKA KWA KUONGOZWA NA HISIA ZA VILE YEYE ASIVYO.
Aliumia na akamwambia Mungu hataki kuendelea, maana hakuomba kuwa umaarufu, wala hakupanga, tena hataki maisha ya namna hii. Ndipo akiwa katika mashauri mengi ya wahubiri wanzie na haelewi somo ghafla akatokea mama mmoja akamsimulia mkasa wa maisha yake akamwambia…. “Mimba yangu iliharibika na nikiwa katika hali mbaya nimekaribia kufa,, nilikuwa nikikusikiliza mahubiri yako siku zile za hatari NA KAMA SIO WEWE KUHUBIRI LEO NINGESHAKUWA NIMEKUFA, KWA HIYO HICHO UNACHOFANYA SIO KWA AJILI YAKO, NI KWA AJILI YETU” Ushuhuda huu ulimfanya aendelee mpaka leo kawa mtu mkuu zaidi katika ufalme wa Mungu.
Yawezekana umekata tamaa, umevunjwa moyo na maisha, mahusiano, kazi, biashara, siasa, cheo, huduma nk. LAKINI NIKUTIE MOYO KUWA KUNA KUNDI KUBWA SANA NYUMA YAKO LINAISHI KWA SABABU YA HICHO UNACHOTAKA KUKIKATIA TAMAA NA KUKIACHA, USIKIKATISHE UTAKATILI MAISHA YAO, MAANA ULIPEWA SI KWA AJILI YAKO, BALI KWA AJILI YAO.
Tafadhari sana usikatishe uhai wako, KWA sababu ya watu wachache, ukajikuta umekata maisha na uhai wa wengi kwa sababu ya hao wachache, okoa wale wanaokupenda kuliko kuwaangamiza wengi kwa sababu ya mmoja aliyeonyesha kutokukupenda. MAISHA YAKO SI KWA AJILI YAKO NI KWA AJILI YAO. USIJIDHURU
CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo…
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!
Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.