Miaka yangu ya kumjua Mungu nimejifunza jambo hili muhimu sana, nimejifunza kwa kusoma maandiko, na kwa kuona kwa macho kile kinachotokea pale imani na utii vinapotumika MAJIBU YANATOKEA.
Kuna wakati mtu anaweza akaponywa/ akapokea/akatendewa na Mungu kwa sababu ya imani ya mtumishi anayemwombea uponyaji. Wakati mwingine mtu hupokea anachohitaji kwa Mungu kwa sababu ya imani yake iliyo ndani yake mwenyewe.
Ndio maana kuna watu Yesu aliwaponya kwa kuwahurumia yeye mwenyewe, ile nguvu iliyondani yake ilikuwa sababu ya watu kupokea. Ila tunaona kuna watu waliopokea kwa Yesu kwa sababu waliamini wakikutana naye watapokea na kupona, rejea habari ya Batholomayo/mwanamke mwenye kutoka damu, na wote AMBAO WALIPOPOKEA ALIWAJIBU KUWA IMANI YAKO IMEKUPONYA.
Tukiachana na utangulizi huo, nataka ujue nini kinaweza kukufanya upokee hasa pale Mungu anataka akutendee na inahitajika imani yako mwenyewe na sio ya mtumishi anayekuombea, halafu wewe ukawa huna imani ya jambo hilo kabisa ila kupokea unahitaji sana. NI KWA NJIA YA KUTII MAAGIZO MUNGU ANAKUPA, KWA KUTII INAMFANYA MUNGU ATAFSIRI UTII KUWA NI IMANI NA KUKUTENDEA. MAANA UNAKUWA UMEIWEKA IMANI KWENYE MATENDO NA KUIFANYA IWE HAI, (Kumbuka imani bila matendo imekufa)
Angalia hadithi ya wakoma waliotumwa kujionyesha kwa makuhani, YESU ALIKUWA HAWAPI ADHABU BALI ULIHITAJIKA UTII WA MAAGIZO YAKE UTAFSIRIWE KUWA IMANI KISHA WAPOKEE.
Petro anaambiwa shusha nyavu, mchana kweupe, tena kilindini, muda ule haukuwa muafaka kupata samaki, mahali hapakuwa muafaka, na taaluma ya Petro ilikataa, uzoefu uligoma. Ndio maana Petro anamjibu Yesu kana kwamba anamwambia haiwezekani kupata samaki sisi tunajua, na ni wazoefu. MAANA YAKE IMANI NDANI YAKE ILIGOMA KUINGIA, ILA KWA KUWA ALIKUWA NA UFAHAMU AKATUMIA KALATA MOJA ILIYOBAKI YA UTII WA MAAGIZO, NA AKAJIBU KWA NENO LAKO NITASHUSHA NYAVU, NA ULE UTII WA KUFUATA MAAGIZO UKAMPA SAMAKI AMBAO HAKUWAHI KUVUA KABLA.
Mfano mwingine ni Naamani aliagizwa na Elisha akajichovye Yordani, mto haukuwa na kitu cha maana, ndio maana walioogelea siku ile kama walikuwa na ukoma au upele hawakupona. ISIPOKUWA UTII ULIHITAJIKA KUITAFSIRI IMANI YA KUMPA UPONYAJI WA UKOMA WAKE NA AKAPOKEA japo alitaka kuleta ubishi, kuonyesha ndani ya moyo wake hakuamini lakini UTII ulimpa matokea sawa na anayeamini na kupokea kwa njia tofauti.
Japo Mimi sio muumini wa maombi yanayoambatanishwa na vitu kama mafuta, chumvi, vitambaa, maji, nk ILA NAKUBALI KABISA VITU HIVI VIKITUMIKA KWA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU, KUIFANYA IMANI IENDE KWENYE UTII NA KULETA MATOKEO NI JAMBO JEMA KABISA( Ila lisiambatane na kutoza malipo, labda kama nayo yameagizwa na Roho Mtakatifu).
NI VYEMA WATU WA MUNGU WAKAJIFUNZA KUTII ILI WAPOKEE. JAPO KWA HALI YA SASA ANAHITAJIKA ROHO MTAKATIFU WAZIWAZI ILI WATU WASIJE WAKAAGIZWA KINYUME NA MAADILI, NIA, MPANGO WA MUNGU, NA KUJIKUTA BADALA YA KUMSOGELEA MUNGU BASI WANASOGELEA MASHETANI NA MASHARTI YA WAGANGA WANAOVAA SUTI. Ndio maana si ajabu kuona watu wanavuliwa nguo na kudhalilishwa kisa wanashida na wanataka kupokea.
Mungu akusaidie kujifunza zaidi ya kile sijakiandika hapa
CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo…
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!
Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.