Baada ya kufa Musa Mtumishi Wa MUNGU wana wa Israel waliomboleza kwa siku 30,baada ya hapo MUNGU alimwambia Yoshua ondoka ,inuka ,vuka mto Yordani wewe na watu hawa wote.
Hebu sikia mtu wa MUNGU Israel wote na Yoshua walikuwa na huzuni,maombolezo,msiba mkubwa Wa Mtumishi wa MUNGU Musa ,kiongozi aliyetegemewa kwenye msafara,wote walichanganyikiwa na kujiuliza maswali itakuwaje kuhusu safari na ahadi za MUNGU juu yao.
Wote walikuwa na hali ya kufanana wote ni wahanga ,ni wafiwa ,MUNGU angaliaye moyo alisema Yoshua alikuwa na moyo wa Hekima ,yaani moyo wa akili ya MUNGU.
Haijalishi unapitia changamoto gani kusudi la MUNGU liko pale pale.
Kusudi la MUNGU ni kuwafikisha Israel Kanani,Mpango Wa MUNGU ni Musa kuwaongoza hadi kanani.
Sasa mpango umekufa njiani yaani MUSA.Ile kwamba mpango umekufa kusudi halijafa ,kanani lazima ufike,Mungu anainua mpango mwingine unaitwa Yoshua anauambia ,Ondoka kati ya waliao,wanaomboleza futa machozi ,tega sikio,kuwa wa tofauti ondoka usiongee kama wao,na pia vuka mto Jordan wewe na watu wote hawa liko wazo la MUNGU ndani yako la kukutoa ulipokwama.
Nasema Mungu akupe mpango mpya ndani yako ili utimizi lile kusudi lako/maono yako.Nasema tena ondoka kati ya wanao lalamika ,waliokata tamaa ,tena ondoka kwanza kifikra na kimawazo ukibadilika kufikiri na kuwaza kwako utabadilika kuongea kwako na jinsi unavyokiri ,chukua hatua ondoka tena vuka ,kikwazo cha hofu,mashaka,kujihukumu ,vuka na sema vuka,wewe ukivuka utabadilisha ukoo wako na taifa zima,ondoka usiwe kama wao vuka ng’ambo ya pili ya uchumi wako,huduma ,elimu ,biashara,ndoa yako,kampuni yako nk .Sasa hivi hawakuelewi achana nao wataelewa ukifika ng’ambo ondoka ,vuka wataelewa na watagundua kuwa umewaacha mbali Mara tu utakapovuka na kwenda ngambo.Tahadhari :usijuvune wala kuwakasirikia ukivuka warushie kamba nao waje,watumie boti waje,wanaojua kuogelea warushie boya waogelee waje, hatuachi mtu hatuachi kitu sote tunakwenda kumtumikia Bwana ,
Kiri sitakaa kwenye madeni naondoka na kuvuka kifungo cha madeni,hasara,magonjwa,kila vikwazo navuka,najua hamnielewi nikivuka mtanielewa tu ,yote yalioibiwa yatakapo rejeshwa Mara saba mtanielewa,miaka yangu itakaporejeshwa mtanielewa tu nasema tutaelewana,najua neno moja tu sasa NIKUONDOKA NA KUVUKA,,Naondoka hajalishi tulilia wote msiba Wa Musa,naondoka haijalishi tuliomboleza wote maana najua ahadi ya MUNGU kwangu haijafa ,Mimi ni Joshua wa nyumba yangu ,Mimi Joshua wa kanisa langu,Mimi ni Joshua wa taifa langu TANZANIA ,Mimi ni Joshua wa Africa,Mimi ni Joshua wa Ulimwengu wote najua hamnielewi Kwa kuwa tunafanana wiwango vya kimaisha lakini subirini nikivuka ng’ambo tutaelewana tu maana MUNGU amenifanya agano la watu ,hivyo dunia nzima inasubiri neno la Bwana toka kinywani mwangu hivyo nasema asiwepo mtu Wa kuzimia moyo hapa maana nakaribia ng’ambo yangu tangu sasa mtu asinitaabishe .Haya ni majira yangu kama na weweni majira yako ondoka hapo vuka mto ,vikwazo vyote mbele yako maana naona umekaribia ng’ambo ziliko baraka zako,Arise,go over …………..
Rise up,.
Yoshua 1:1-3,5-6,ISAYA 60:1
[1]Ikawa baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema,
[2]Musa mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka, vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa Israeli.
[3]Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.
[5]Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.
[6]Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
Isaya 60:1
[1]Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,
Na utukufu wa BWANA umekuzukia.
CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo…
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!
Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.