Siku za mwisho kutakua na njaa.(Amosi 8:11)

Kwakua watu wengi sio wasomaji wa biblia basi wao hukalili njaa basi wamemaliza ndio maana kuna mwaka fulani ilitokea njaa kali watu wakasema ni mwisho wa dunia kwakua hata Biblia imesema hivyo wakafanya maandalizi mengi ya kufa lakini hawakujua njaa inayo zungumzwa hapa ni njaa ya neno la Mungu na sio neno tu bali neno halisi.

Ulimwengu wa leo kumekua na makapi sana yaani sio kila anaye hubiri au kusema habari za Mungu ni za kweli makanisa mengi yanatumiwa na shetani kutisha na kupotosha watu wa Mungu,makanisa mengi yanawafanya watu wasiwe na tumaini na Mungu yanawaonesha kama hakuna haja ya kuomba baraka wala kuwa na tumaini hivyo basi watu wengi wamebaki kuwa tegemezi wa kusikia sio kusoma kweli ya Mungu.

Huwezi kufaulu mtihani bila kusoma haiwezekani mtu aje akusimulie tu na wewe useme umejua ndio maana unadanganywa mimi kazi yangu ni kuja kusema kile Mungu amenituma kama nitaongopa utajua kwakua wewe pia unalijua neno hakuna sehemu kwenye biblia panazungumza anayefaa kusoma biblia ni mchungaji peke yake hapana.

Mungu akupe neema ya kumjua kama unataka kuajiliwa na kampuni fulani lazima ujue habari za hiyo kampuni ndivyo unavyotakiwa kufanya kama unataka Mungu akupe uzima au akutoe kwenye shida yako lazma umjue kwani kila shida kuna namna na njia ya kushinda sio kila tatizo tunakemea mengine ni mpaka uongee na Mungu kwa unyenyekevu ndipo yatoke.
Inawezekana matatizo mengine ni wewe umesababisha,ukoo wako ndio uliingia kwenye maagano na shetani sasa unakemea nini unahitaji uongee na Mungu akupe passwords ili upite hapo.Natamani ulijue neno la Mungu kwani hutapata shida.

CantonaJoseph’s contacts

Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/

Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.

Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph

LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo

Management Fortune Baraka Entertainments

Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com

Email:fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com

cantona.online254@gmail.com

Contacts +254748836127

Wewe ni wa maana sana!

All Rights Reserved @2019/FortuneBarakaEntertainments.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment