Tetea Imani yako.

HALELUYA WANA WA UFALME

Leo ni siku njema kabisa aliyoifanya Bwana kwa ajili yetu, tutaifurahia na kuishangilia

Ninakukaribisha tena kwenye mwendelezo wa somo letu lenye kichwa kinachosema TETEA IMANI YAKO.

Hii ni sehemu ya tano.

Na msingi wa somo letu ni Habakuki 2:4 Lakini mwenye haki ataishi kwa IMANI yake

IMANI NA KUONA

2Wakorintho 5:7… Maana twaenenda kwa IMANI, si kwa KUONA

Mungu alimuumba mwanadamu aishi kwa IMANI na siyo kwa KUONA maana imeandikwa “Lakini mwenye haki ataishi kwa IMANI yake – Habakuki 2:4 “.

IMANI ni kazi ya moyo na KUONA ni kazi ya macho

Mtu anayeishi kwa KUONA, ni yule anayesubiria aone jambo limekwisha fanyika au limekwisha kuwa dhahiri kwenye maisha yake kwanza ndipo achukue hatua ya kuamini.

Watu wa namna hii wanaishi maisha ya hali ya chini sana, na huchukua muda kufanikiwa katika mambo yao wanayoyafanya. Na kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kupokea kutoka kwa Mungu, kwa sababu Mungu mwenyewe anaishi huko kusiko onekana na bila kuenenda kwa IMANI huwezi kupata huduma kutoka kwake.

Kinachoonekana ni kikwazo kwa mtu anayetaka kuishi kwa IMANI, kwa sababu sheria ya imani adui yake ni kinachoonekana.

Imani ni maisha ya rohoni na ni kanuni ya rohoni ila inafanya kazi katika mazingira yanayoonekana kabisa, hivyo wanaoenenda kwa kuona hawawezi kupokea kutoka kwa IMANI, kwa sababu IMANI inamtaka mtu amini bila kujali ukweli na uhalisia wa kile kinachooneka kwenye mazingira halisi.

IMANI inamtaka mtu anayepuuza ukweli unaoonekana na kusimamia UKWELI aliosema Mungu kwenye neno lake ambalo ndio IMANI.

IMANI ni kile alichokisema Mungu kwenye NENO LAKE, yaani kwenye BIBLIA. Anayelitumia NENO LA MUNGU kama kipimo katika maisha yake, bila kujali kinachoonekana huyo ndio anayeenenda kwa IMANI.

Unapoamua kusimama na kulitegemea neno la Mungu huku ndiko kuenenda bila kuona. Watu wanaoenenda kwa KUONA ni wale wanaoenenda kwa kusikia, kunusa, kugusa na kuona na watu wa IMANI wanamwamini MUNGU tu bila kujali chochote kile walichokisikia au kukiona au kukigusa n.k

Wanaoenenda kwa KUONA, wanaishia kushindwa, kutaka tamaa, na kuona hawana tumaini tena kwenye maisha yao. Wanaoenenda kwa KUONA wanajiona wao na wale wanaowatumainia, lakini wanaoenenda kwa IMANI wanamwona MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, ndio maana mtume Paulo akasema tunaenenda kwa IMANI na siyo kwa KUONA.

Kwa leo tuishie hapa, tukutane sehemu ya sita…

Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo akubariki sana na Ukafanikiwe kwa kila ulitendalo …. AMINA

©2019 Reserved|Fortune Baraka Entertainments
©


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment