Shetani anaweza kuwa amepindisha maisha yako mwamini Mungu utapona

Luka 13:10-12

Siku ya sabato alikuwa akufundisha katika sinagogi mojawapo, (11 ) Na tazama palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane,naye amepinda hawezi kujinyoosha kabisa. 12 Yesu alipomwona alimwita,akamwambia mama umefunguliwa katika udhaifu wako.

Haleluya!!!

Habari hizi ni mwanamke aliyekuwa na udhaifu wa kupinda kwa mda wa miaka kumi na minane,
Shetani alipindisha maisha ya huyu mama ,akaishi kwa mateso mda mrefu ,lakini siku aliyokutana na Yesu ushindi ukawa sehemu ya maisha ya yule mama.

Inawezekana na wewe ni sawa na yule mama kwa Habari ya maisha yako.

unapitia shida nyingi, umejawa na uchungu tele moyoni mwako, shetani amepindisha maisha yako,afya yako, ndoa yako.

Hali yenye inakufanya ukose imani hata ukate tamaa.

Asubuhi ya Leo Nakutangazia Uponyanyaji katika jina la Yesu.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment