Kila mtu ambaye nyota yake inawaka, lazima awe na maadui wakuipinga,ukiona hauna anayekupiganisha,ukiona hakuna anayekusema mabaya katika vikundi vya watu,ukiona husengenywi,iwapo hakuna anayekejeli mipango yako au kupinga mipango yako jua hauna nyota,ukiwa na nyota lazima wainuke watakaokupinga na kuzima nyota yako.Yusufu katika kuinuka kwake alikua na maadui ndugu zake walioipinga nyota yake,waliinuka na vikwazo vingi kuzima nyota yake,mke wa potifa naye alijaribu kuzima ndoto yake. Lakini Mungu ainuliwe walipofikiri wana muuza misri kuzima ndoto yake ndipo walimsindikiza kufikia kusudi la Mungu.
Annah alidharauliwa na Mke mwenza Peninnah pasipo kujua,Mungu ana mpango naye,Annah aliomba mtoto naye Mungu alikua anataka Nabii. Huyu Mungu ni Mungu wa miujiza.
Endelea kumtumainia Mungu kwa lolote unalolifanya Maishani.Leo hii iwapo hauna maadui fahamu fika,kwamba ndoto yako ilizimwa kitambo iwapo hauna wanaokusema vibaya hauna la kuwaeleza.Adui anajua kunusa ukuu, Mungu anakuandalia ili apige vita nyota yako.Heri mtu yule ambaye ana mtumainia bwana ni kama mlima sayuni ambao hautayumbishwa hayo majira yakija utadumu milele.

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.