Mungu anaenda kufungua ukoo

Kuna mambo mengine yameanza umeyakuta lakini wewe hukuyaanzisha,kuna magonjwa kwenye ukoo wako,laana hata wewe hujui ni nani na ni wapi zilianzia lakini matatizo yapo.Kuna wakati, Mungu ameruhusu hayo mambo kwakua anataka ajitukuze kwa hayo kupitia wewe unaye mkiri Yesu itapita nguvu ya Mungu na kufungua ukoo wako ili Mungu akatukuzwe kupitia wewe.
Kama mtu anaweza kuzaliwa mara ya pili basi tambua hata uumbaji unaweza kufanyika mara nyingine kwenye maisha yako,pale palipo haribika iwe ni Afya,Uchumi,Kazi,Ndoa,Familia wiki kabla ya kuisha Mungu anakwenda kuumba tena.
Sio kila anayekuja kwenye maisha yako ana maana wengine wamekuja kuharibu maisha yako
Ni kama balb iwakavyo usiku wadudu mbali mbali husogea lakini wengine huigonga iyo balb pamoja na kwamba inawapa joto na nuru,wengine huichafua balbu.
Usiogope asema Bwana,watu wanaoshindana na wewe wata angamia,na kuwa si kitu
(Isaya 41:10-12)
Maisha mabaya unayo ishi leo tambua kuna mtu kasababisha,kama vile mfalme Daudi alipoona Mvua hainyeshi miaka mitatu akaenda kumuuliza Bwana naye akamwambia ni Sauli kasababisha maana aliwaua wagibeoni (2Samweli 21;1….)Naingia kwenye maombi tena kwaajiri yako niambie nini kimekuzuia nami nitamuuliza Mungu ili tujue chanzo yawezekana mababu zako waliingia maagano ya giza hizo madhabahu zimepata uhalali wa kutesa maisha yako,leo kuwa na uchungu nami nitaomba kwaajiri yako.
Labda umekua ni mtu wa kujilaani tu mwenyewe kuanzia jua limetoka mpaka linazama umekua ni mtu wa kuhukumu na kusema maneno mabaya,hujawahi hata siku moja kumshukuru Mungu aliye kuumba ndio maana mpaka leo hujajua kusudi lako ni lipi.Mungu ana haja na wewe kunijua mimi ni mpango wake ili nikuvushe nina omba kwaajiri yako na utafanikiwa kwa Jina la Yesu.
Inawezekana watu hawakuthamini,wala hawaoni kama utafanikiwa lkn Mungu kaweka jambo la siri ndani yako ambalo litawashangaza wote na wale waliokukataa watakutafuta na kuomba uwasidie.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment