Muhubiri mmoja mkubwa ambaye alifika hatua ya kuacha anachokifanya.
Anasema yeye hakuomba kuwa maarufu, ila kile alichopewa kufanya kilimpa umaarufu, na Kwa sababu ya umaarufu huo siku moja alishambuliwa na kuandikwa vibaya na gazeti,
na kama ilivyo kawaida hakuweza kujitetea wala kusahihisha kuhusu tuhuma na kashfa waliyomwandika,maana waliomwandika hawakujali usahihi wa vile alivyo,bali waliandika kwa kuongozwa na hisia.
Aliumia na akamwambia Mungu hataki kuendelea, maana hakuomba kuwa umaarufu, wala hakupanga, tena hataki maisha ya namna hiyo. Ndipo akiwa katika mashauri mengi ya wahubiri wanzie na haelewi somo ghafla akatokea mama mmoja akamsimulia mkasa wa maisha yake akamwambia…. “Mimba yangu iliharibika na nikiwa katika hali mbaya nimekaribia kufa,, nilikuwa nikikusikiliza mahubiri yako siku zile za hatari na kama sio wewe kuhubiri leo ningeshakuwa nimekufa.
Ushuhuda huu ulimfanya aendelee mpaka leo kawa mtu mkuu zaidi katika ufalme wa Mungu.
Yawezekana umekata tamaa, umevunjwa moyo na maisha, mahusiano, kazi, biashara, siasa, cheo, huduma na kadhalika. Lakini nikutie moyo kuwa kuna kundi kubwa sana nyuma yako linaishi kwa sababu ya hicho unachotaka kukikatia tamaa na kukiacha,usikatishe utakatili maisha yao,maana ulipewa si kwa ajili yako,bali yo,bali kwa ajili yao.
Tafadhari sana usikatishe uhai wako, Kwa sababu ya watu wachache, ukajikuta umekata maisha na uhai wa wengi kwa sababu ya hao wachache, okoa wale wanaokupenda kuliko kuwaangamiza wengi kwa sababu ya mmoja aliyeonyesha kutokukupenda.
Maisha yako si kwa ajili yako,ni kwa ajili yao.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.