Ifanyie maandalizi imani yako kwa kuipalilia ili muujiza wako ukaonekane kwa Jina la Yesu

Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kama BWANA angewatia roho yake.
Ndugu wakae pamoja kwa umoja.
Natamani kusema kama Musa alivyosema
Hesabu 11:29
Nami nasema njia pekee ya kukomesha roho ya wivu ni kutaka watu wote wawe kama wewe, waimbaji kama wewe, wazuri kama wewe, matajiri kama wewe, waliofanikiwa kama wewe. KUWAONEA WIVU WENGINE AU KUWARUHUSU WENGINE WAONE WIVU KWA SABABU YA NAFASI YAKO NI KUJIANGAMIZA MWENYEWE. PENDA NA WAFANYE WATU KUWA KAMA WEWE.
Inawezekana watu hawakuthamini,wala hawaoni kama utafanikiwa lakini Mungu kaweka jambo la siri ndani yako ambalo litawashangaza wote na wale waliokukataa watakutafuta na kuomba uwasidie.
Kuna mambo yanaweza kukuvuruga mpaka ukisikia neno la Mungu unaona ni uongo yawezekana umesha kutana na madaktari bingwa wakakuhudumia lakini hujapata nafuu,au umeshatembea sana kutafuta msaada lakini hali yako bado iko pale pale,Musa wakati anakwenda kuwaokoa wana wa Israel farao alipojua akaongeza adhabu na uchungu ukazidi kwa wana wa Israel wakamlalamikia Musa “kama kweli Mungu kakutuma utuokoe mbona mateso kwetu ndiyo yanazidi?” waliona kama ni uongo lakini Mungu si mwanadamu hata aseme uongo alisema atawatoa misri wao na mali zao na watoto wao na mifugo yao.Nami nasema Mungu anakwenda kujibu shida yako ambayo imekupa huzuni na uchungu,shida iliyokufanya ukate tamaa,shida iliyo rudisha imani yako nyuma,kupitia kipindi channel leo katika channel hi ya CantonaCast TV. Fahamu,

Imani ni kama Moyo au Roho huwezi kumpa mtu akubebee shida uliyo nayo,ugonjwa unaokutesa miaka mingi au hali ngumu ya maisha haiwezi kutoka kama wewe hautaamua inahitajika imani ili kusababisha hali hiyo ipotee kabisa,huwezi kumpa mtu ugonjwa wako wala huwezi kumpa mtu shida zako lakini ukiwa na imani mizigo ya shida zako utampa Yesu kwakua yeye amesema njooni kwangu mnaoelemewa na mizigo.

Wakati Paulo na Barnaba wanakimbilia Lista huenda watu walidhani wao ni waoga lakini kumbe Mungu aliwapeleka huko ili wakakutane na kiwete ambaye hajawahi tembea tokea kuzaliwa kwake ili Mungu akamponye,kusudi la Mungu aliloweka kwangu ili kupitia mimi ukafanikiwe.

Natangaza rasmi utafanikiwa endelea kumtumainia bwana.

Wakati fulani Elisha alimuombea mama mmoja akapata mtoto lakini baadae yule mtoto akaugua kichwa akafa,mama yake akamchukua na kwenda kumlaza juu ya kitanda alichokuwa ana lala Elisha mtu wa Mungu,kipindi wanafunzi wa Yesu wanahubiri wagonjwa waliletwa juu ya vitanda ili Petro atakapo pita angalau kimvuli chake kiwaguse wapate kupona,Yesu aliombea wagonjwa walioletwa kwenye vitanda na magodolo.Kitanda kinafananishwa na imani unapokuwa umechoka na mizunguko ya siku nzima unakwenda kulala kitandani,kitanda ni Imani unapo kuwa na shida imani yako itakupumzisha utakua ukiamini Yuko Mungu wa kuniweka huru.Wacha Mungu akakutende mema unapoendelea kutazama CantonaCast TV empacting families,hub of hope.
A production of FortuneBaraka Entertainments.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment