Kuwa maskini si tiketi ya kutojituma na kuwa tajiri si tiketi ya kuwanyanyasa wanyonge.Wakati fulani,maishani maskini hana hoja,walisema wahenga wa kale.Muhenga ni mzee aliye na busara kwa sababu si kila mzee ana busara maana hata hata wajinga wanazeeka.
Maskini wakati fulani,hawaminiki hata penye vikao vya familia,maskini akinyoosha mkono kuchangia hoja,ndugu watadhani anataka kuzua fujo. Ukiwa maskini,unaweza kuumwa hata na umbwa wako.
Hebu niseme hivi umaskini ni kuadhibiwa kwa kosa ambalo hujatenda au umelitenda kwa kupoteza fursa nyingi,ambazo ulizipata.Pamoja na balaa la umaskini Kuna wanaoamini umaskini ni sehemu yao hamna haha ya kujituma.Maana imeandikwa rahisi ngamia kupenya tundu la shindano kuliko tajiri.Hiki ndicho kifungu maskini wanatumia ndiposa wengi wanachezea fursa wanazopata,wanafarijika Sana na kuwa maskini.
Ukiwa maskini hata akili huwa nzito,kuelewa mambo katika uhalisia wake.Na kutawaliwa na dhana fedha ni chanzo cha maovu.Wakati unadaiwa kodi,unadaiwa ada,unadaiwa rejesho,unadaiwa hadi zaka na sadaka.Ukihitaji matibabu hauna fedha je utasaidika vipi?,ukiwa na fikra za umaskini,utasema fedha ni chanzo cha maovu,lakini ukiwa na fikra za utajiri utasema utasaka pesa ili ukwepe balaa,na upweke maana tajiri hujijengea marafiki,hapa utapata msemo nyumba ya tajiri haikosi wageni.Maana marafiki wake ni wengi tajiri anamtawala maskini soma methali 19:4
Maskini anafikra ya kufanikiwa pasipo kufanya kazi,maana imeandikwa omba na utapewa.Tajiri anafikra ya kufanikiwa kwa kupiga kazi,maana imeandikwa asiyefanya kazi na asile.
Maskini anadhana,kila tajiri ni mwizi na anawadhulumu wanyonge na tajiri anadhana kila maskini ni mvivu na hapendi kufanya kazi Soma methali 21:25-26.
Maskini hudhani,ili ufanikiwe sana lazima usome sana ,maana imeandikwa mkamate elimu usimwache aende zake,ndio maana maskini huekeza katika elimu ya watoto wake atauza chochote mtoto asome afikie viwango vya juu, swala ambao hapa huzaa matunda.Maskini atalala njaa lakini mtoto asome.
Tajiri anawaza uwezo wa kufanikiwa ni kutawala rasilmali zilizopo na kuzifanyia kazi,anafwata kifungu nendeni ulimwenguni mkamiliki,kutomiliki Mali ni kuping’ana na agizo la Mungu.
Kwa maskini kazi ni adhabu,kwa tajiri kazi ni burudani,maskini hutegemea pesa kwa kazi ambayo hapendi ndio maana anachukia kazi,kwa tajiri anatengeneza pesa kwa kazi anayoipenda ni burudani kufanya kazi.Tajiri analala masaa machache Sana, maskini analala masaa mengi na kuchelewa kuamka,ana amini matajiri wote ni washirikina.
Tajiri ana amini maskini wote ni wavivu,ndio maana wananyanganywa hata kidogo walicho nacho.Soma matayo 25:29.
Wenye fikra za kitajiri hupanda miti ya mbao na wenye fikra za utajiri wao hupanda mchicha.Maskini huamini binadamu wote ni wabaya na dunia yote imeoza,tajiri anaamini binadamu wote ni mtaji na dunia ni fursa.
Maskini anafunza watoto wake jinsi ya kupambana maishani maana maisha ni mapambano. Tajiri anafunza watoto,kuenenda na akili.Maskini anapambana kwa kila Jambo,,maana hajapangilia Mambo yake hata akipata fedha nyingi huenda akajutia au zikamwangamiza.Akipita mjini ananunua kila kitu anachokutana nacho akiwa na hela.Maskini ni mdogo kuliko matatizo yake.
Tajiri huomba Mungu na kujituma,maana Mungu anawapenda wote,maskini na matajiri tumeumbwa kwa mfano wake.
Tafuta utajiri kwa bidii maana ni Mungu anapeana fursa kwa mtu yeyote.Yesu kristo alikuja duniani ili tusihangaike tena Soma Wakorintho wa pili 8:18
Kukataa utajiri kwa kuwa mzembe ni kukataa upendo wa Mungu ambao unataka ufanikiwe kwa kila Jambo unalolifanya. Ukikataa utajiri unakwepa majukumu ya uongozi uliopewa na Mungu shambani mwa Eden,tutawale vyote vilivyomo duniani.Nchi na vyote vijazavyo ni Mali ya Mungu.Usisome biblia kutia watu hofu watu wewe.Muhudumu katika nyumba ya bwana,wafunze watu waelekeze kulijua neno na litawaweka huru.Asiyefanya kazi na asile,mshirikishe Mungu katika Jambo lolote unalolifanya,usipomshirikisha Mungu huenda hiyo kazi ikakudhuru au ikakufaidisha iwapo utamtanguliza Mungu kwa Hilo unalolifanya.Wengi wamepata kazi ikawaletea madhara wakati walikosa kuweka Mungu mbele.Tunaishi kwa neema.Yohana 15.
Wenye fikra za kitajiri husema nayaweza Wafilipi 4:13-14. Tafuta ufalme wa Mungu na haya yote utazidishiwa.Unapigwa na umaskini kwa sababu ya kutoliheshimu neno.
Hagai 2:8,kuwa na pesa au Mali si dhambi.Abraham alikua tajiri 13:2,Ayubu alikua tajiri 1:3,Yusufu wa Arimathea alikua tajiri matayo 27:57-60
Shetani anafahamu ukiwa tajiri injili itawafikia wengi.Nakuombea uwe tajiri,ule mema ya nchi.Amka uanze kufanya kazi.Usilalie msumari usiende kulalia fursa.Matatizo ambayo unakumbana nayo leo hii utayatatua wewe mwenyewe.Amka saka fursa yako,chakarika kila pembe utafanikiwa.Jitunze kwa walioranikiwa na soma vitabu vwa kufanikiwa vitabadili msimamo wako,si mda utafurahia utakayo yaona.
#Iposiku #GetInspired #TwapigaHatuaPamoja #ImpactingFamiliesTheHubofHope. #CantonaJoseph’World. #CantonaJosephIntMinistry. #CantonaJosephMotivates.
Links
Tweeter @cantonajoseph
Facebook Cantona Joseph
Instagram cantona.joseph
Youtube CantonaJoseph Joseph Official
YouTube CantonaJoseph Int Online Media.
©2019 Fortune Baraka Entertainments
All rights reserved.

FortuneBaraka Photography

FortuneBaraka Photography 
FortuneBaraka Photography
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.