Upo kwenye umri upi?

Mwanadamu anapozaliwa ni mfano wa msafiri aliye bandarini,sekunde inaposonga hubadili dakika,masaa siku,juma mwezi miaka ambapo katika hatua anayopiga ina ubora wake na changamoto pia.Unapotumia mda wako vizuri,unajijengea nafasi ya kutojutia miaka ya uzeeni.Leo hii,nitakunasihi umuhimu wa umri, keti mkao wa kupokea hilo.

Mwaka wa 1-13.Hiki ni kipindi mtoto anakua hapa anataka kufahamu mambo mengi,yanayomzunguka katika mazingira aliyomo.Hapa mtoto ana maswali mengi sana,ambayo hayana kikomo.Wengi wanaiga mambo mtu mzima anayafanya.

Mwaka 14-45.Miaka ya ujuaji mwingi.Anapo balehe anaanza kuingia na hulka anajua saana,wacha niwafahamishe hili au lile.Anajua kila kitu,hapa haitaji maelezo la kufanya jambo vijana wengi hapa utagundua wanabishana kijiweni najua,najua hata Kama hajui.Wengi hupoteza nafasi za kujijenga katika kipindi hicho masomoni,kazini na katika taaluma.Wanapoteza pesa kwa anasa pasipo kujiwekea misingi ya uzeeni.Wakipata mtaji wanautumia vibaya.

Miaka 46-59 ni miaka ya majuto.Umri unaenda anawaza la kufanya,hajaekeza mahitaji mengi pesa za matumizi hazipo.Hajajenga nyumba vijijini angali anaishi katika vyumba vwa kukodi.Watoto wanaitaji karo.Semi ninge,ningefanya nikiwa na hela,ningefanya.Ninge.Semi zake ninge-ninge.Hii inakua miaka ya majuto. Hapa utawapata walioajiriwa wakiwa katika kipindi hiki wanapenda rushwa kuokoa mda waliopoteza.

Miaka ya 60-70 na kuendelea miaka ya waliokata tamaa,hapa anauza hata kipache cha ardhi alichopokezwa na baba yake kijijini semi zake nikifa msinipeleke vijijini.Nikifa hana neno la busara kuzungumza na wajukuu hana watakacho Soma kutoka kwake.Kitabu chake cha maisha kilijaa dosari hadi hamna la kuwaelimisha familia yake.

Maisha ni kitabu mhusika mkuu kukinakili ni wewe, mhariri mkuu ni wewe.Maamuzi utakayofanya leo yatakujengea sifa siku za uzeeni wakati nguvu unazo zitakua zimepungua.

Jiandae ungali kijana.Ule na Uma a kijiko uzeeni pasipo kuhangaika na mahesabu ufanye nini,Wala kuwalaani watoto waking wasipokusaidia.

#Iposiku.#GetInspired. #TwapigaHatuaPamoja. #CantonaJosephMotivates. #CantonaJoseph’sWorld. #CantonaJosephIntMinistry


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment