Nguvu ya Upweke

Siku zote wanadamu wapo tuu,Wanaume wapo tuu,Wanawake wapo tuu,atakupenda iwapo unadhamana,atakudhamini iwapo umejijengea dhamana yako.Katika maisha ni bora wakati mwingine kuwa pekee yako maana katika mazingira hayo utajijengea dhamana yako. Mambo makubwa hayajafanyika wakati upo katika vikundi vya marafiki.Ukiwa pekee yako una mda bora kupanga mambo yako.Ni wakati bora kutambua wewe ni nani,ni wakati bora uanze wapi,utatumia mda mwingi kufikia unachokihitaji maishani.Utafanikisha malengo yako.Utatumia mda mwingi kujiuliza uende wapi,tofauti ukiwa na marafiki,mtacheka mtafurahi huku ukifanya wanachokisema pasipo maamuzi yako.Tofauti na unapokuwa pekee yako,kama ulivyozaliwa pekee yako.Ndipo utagundua inafaa uanze safari ya wewe pekee yako,utoke hapo ulipo.Marafiki kukutenga lisikukoseshe usingizi.Chukua hatua,hapo ulipo Jenga dhamana yako.Unapotengwa ndio mda sahihi wa kujijengea dhamana yako.

#Iposiku. #Getinspired #CantonaJosephMotivates. #CantonaJosephWorld. #TwapigaHatuaPamoja

Allrights reserved ©2019


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment