Jifunze kukaa katika vikundi vya watu wenye mtazamo chanya,maana watakutoa kutoka sehemu moja kufika sehemu nyingine Bora uwe mwenye subira na kumwamini Mungu muumba wa mbingu na ardhi.Hatima yako ipo,katika kusikia kwako.Jifunze namna ya kusikia ndani mwako.Maana kusikia kwako hapo ndipo hatima yako,akasema baba mzazi mzee wangu Benjamin Endesha.Usiku huo nilimsikiliza tena kwa makini akinipa ushauri huu.Aliendelea”wakisema hauwezi,zungumza na nafsi yako,sema naweza,wakisema haufai sema tuu nafaa,wakisema hautafanikisha jambo,piga moyo konde,sema na nafsi yako nitafanikisha.Kipindi hicho nilikua na umri wa miaka kumi na saba,nikiwa kijana barubaru,mwenye mawazo mengi mbona baba kasema hivi, nililishika sana hili neno.”Mwanangu Cantona Joseph wewe ni babu yangu maana babu yangu aliitwa Joseph,alikua mtu mkakamavu saana siku za uhai wake,ujasiri huo nauona ndani mwako nakupenda mwanangu,wewe ni nguvu zangu mwana wa ujana wangu,nguvu zangu za kesho.Maneno ya watu yenye mtazamo tofauti,yasikufanye urudi nyuma.Jifunze kusikia,marafiki unaotembea na kushiriki nao watakujenga au wakubomoe,nakuombea mwanangu mema katika dunia hii ambayo haina mazingira rafiki,tembea na marafiki walio na mtazamo chanya.Hatima yako naiona ipo katika kusikia kwako,unachokisikiliza kitakutengenezea mazingira salama.Wakisema hauwezi,hufai au hautafanikisha hili ama lile.Jiambie moyoni nitafanikisha hilo.Namna yako kusikia ni baraste ya ufanisi wako.Nakuombea dua,utakapokumbana na mlima wa changamoto nifahamishe nitakuombea dua kwa Mungu”Akasema mzee wangu Benjamin Endesha.Haya maneno yananipa ujasiri kujielewa na kuendelea kukwea milima maishani,hamna jambo ninalolifanya kwa kupurupuka naliwaza kabla kutenda, nikifahamu fika kwamba ninachokisikia kina nipa mafunzo na ndani kwa ndani nasema na nafsi naweza.Hili nalo litapita.Nawe jifunze kukaa na watu wenye mtazamo chanya.Ndoto zako zitatimia.
#Iposiku. #Getinspired. #CantonaJosephWorld. #CantonaJosephMotivates. #CantonaJosephMotivate #TwapigaHatuaPamoja.
All rights reserved ©2019

FortuneBaraka Photography

FortuneBaraka Photography.
Kipindi kile nikiwa barubaru, maisha ni safari.
Nilipohadidhiwa semi hizi nzito.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.