Wewe una umri mkubwa kuliko umri wa dunia usijidharau. Ndani ya wazo la mungu ulianza wewe ndipo akatanguliza dunia,kuonekana ili ikuhudumie wewe.
Kabla yako alitanguliza tumbo la mama ili likuhudumie wewe, alikujua tangu tumboni mwa mama Yer 1:5 Hivyo kabla chochote ,unachokijua,wewe ulishajulikana,usiogopeshwe na unachokijua jiheshimu ulianza kujulikana na Mungu.Usijidharau mazingira uliopo,familia yenu,na Yale unayopitia yasikukatishe tamaa.Endelea kumtumainia aliyekuumba.
Na alikuchagua kabla ya misingi ya dunia kuwepo Eph 1:4-14 Kabla hajachagua aumbe nini,wewe tayari ulishachaguliwa hivyo usiogopeshwe chochote,ulishachaguliwa wewe ni bosi hivyo ulitangulia kwenye wazo la Mungu,kabla ya lolote.
Na alikutakasa kabla ya misingi ya dunia kuwepo Rum 8:29 Usijihesabie hatia ambayo yeye alishaiondoa kupitia msalaba, aliposulubishwa kristo,pasipo ya hatia. Wewe ni wa maana Sana kwa Mungu.
Usitishwe na kinachotangulia kuonekana kiwe kizuri au kibaya jambo la muhimu kwako ni wazo la Mungu ambalo hufuata,kuonekana baada ya wazo la Mungu,ambalo hufuata kuonekana baada ya mazingira ya kubeba wazo hilo kuonekana.Usijidharau wewe NI mtu was maana machoni pa Mungu.
#Iposiku #GetInspired #CantonaJosephMotivates
#CantonaJosephWorld
All rights reserved ©2019

CantonaJosephMotivates
FortuneBaraka photography
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.