Wakati Meshaki,Shadrack na Abednego wanatupwa katika tanuru la Moto sio kwamba ule moto ulikua hauogopeshi ulikua unatisha sana lakini walikua wanamuamini Mungu wakijua atawaokoa,wakati Daniel anatupwa kwenye tundu la simba sio kwamba simba walikua wametulia hapana walikua wakinguruma na aliona kabisa kulikua na mifupa ya watu wengine waliokuwa wameliwa baada ya kutupwa humo ndani lakini alikua na imani na Mungu hata akiliwa na simba atakwenda mbinguni kwa Baba,ebu jaribu kumuamini Mungu kwa jambo ulilonalo usikimbie jaribu ukiweka uoga na kujaribu kwa akili zako kuokoa nafsi yako utaipoteza ila uki jihatarisha maisha yako mbele za Mungu utayaokoa pita hapo hapo kubali kutupwa kwenye tundu la simba utamuona Mungu akituma malaika wake,kubali na uende hapo ndipo utauona ushindi usiumizwe na maneno yao wala ugonjwa ulionao Nakuombea Mungu akuokoe.Pale unapofikia mwisho ndipo Mungu hutokea na kutoa msaada
Tafsiri halisi ya kuishi ni kukopeshwa uhai.Mungu ametuleta Duniani kwa mpango maalum haujakuja uishi tu kisha urudi mbinguni hapana kuna jambo unalijua ambalo mwingine hawezi kulifanya na Mungu anakuamini wewe akijua kupitia wewe kile alicho kiweka ndani yako kitakua faraja na msaada kwa watu wengine,sasa hivi wewe ni mzima ni kwa sababu ya Neema ya Mungu iko juu yako Mungu amekuacha hai ili ulipe deni umeamka salama wengine ni wagonjwa unaishi vizuri wengine wana shida nyingi.Tumia muda wako vizuri na utengeneze njia yako na Mungu kwani wote tumeumbwa na Mungu na mwisho wa siku tutarudi mavumbini na tutatoa hesabu ya deni la uhai.Naachilia Neema ya Mungu juu ya Maisha yako upate kila unachostahili na ukauguse moyo wa Mungu.
#Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates
All rights reserved ©2019

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.