Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja.

Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu (Isaya 4:1)
Moja kati ya maswali ninayo ulizwa sana watu wakitafsiri kwamba andiko hili wanawake watakosa kuolewa mpaka watakua wengi kiasi kwamba wanawake 7 watamng’ang’ania mwanaume mmoja, SI KWELI
Andiko hili ni ufunuo kutoka kwa Nabii Isaya,maana ya neno hili ni kwamba nyakati hizi tulizopo kiBiblia ni nyakati za mwisho yaani nyakati ya saba,Isaya ni nabii aliye ishi karne ya nane K.W.K alitabiri mambo mengi miaka maelfu iliyopita maana ya neno hili ni kwamba katika nyakati hizi yatatokea makanisa ambayo yatakuwa yanafanya mambo kwa mfumo wao na kutoa mafundisho kwa utashi na ufahamu ambao sio wa KiMungu lakini watatamani walitumie Jina la Mungu.Hawatafanya ibada za kweli lakini wanalitumia Jina la (Mungu,Yesu) wanafanya miujiza kwa nguvu zao lakini wanalitumia Jina la Yesu.Na kuna watu ni washirikina lakini wanakwenda kanisani tena misa ya kwanza ili tu watu wanaomzunguka waone kuwa anasali,wanafanya hivyo ili kuficha wasingundulike kwa urahisi.Lakini neno linasema katika (Isaya 4:2)Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa nzuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya wale waliookoka.Siku hizi ni siku za Neema kwako wewe uliye okoka,ni siku za baraka kwako wewe uliye okoka,ni siku za kumtukuza Mungu kwako wewe uliye okoka.Mungu akakupe nguvu na maarifa ya kumjua na kutambua namna iliyo bora ya kumuabudu Yehova.

Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates All rights reserved©2019


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment