Kila mtu unayemuona duniani Mungu aliruhusu awepo kwa kusudi maalum. Ndiyo sababu kila mtu alizaliwa siku yake, saa yake na kwa namna yake .Hata mapacha hubishana muda wa kuzaliwa na mama anayejifungua mapacha atakwambia kila mtoto ana uchungu wake.
Hii ni kwasababu baada ya kuzaliwa Mungu alitaka kila mtu awe na maisha yake na atekeleze kusudi alilowekewa ndani yake. Ila imekuwa tofauti sana na vile Mungu alivyokusudia kutuweka duniani.
Kutokujiamini/Kutokujikubali.
Hii ni hali ambayo inawakumba wengi wanapofikia wakati ambao wanafaa kujitambua na kutumia uwezo ule ambao Mungu ameweka ndani yao. Hii ni kwasababu wanajifananisha na watu wengine ambao wamefanikiwa pasipo kufahamu walianzaje. Hivyo inawasukuma wao kutaka kuanza kutumia uwezo ulipo ndani yao na kupata mafanikio kwa mara moja. Ni kweli mafanikio yapo katika kufanya kile ambacho Mungu ameweka ndani yako ila yanakuja hata kwa hatua .
Pia wengi hukwama kwa kufuata ushauri mwingi kwa watu wa karibu na kusahau kufanya kile wanachoweza kufanya kwa usahihi wote.
Fanya Hivi.
Tambua upo duniani kwa kusudi maalum, jiamini kwamba Mungu ameweka uwezo ndani yako wa kufanya mambo. Usikubali watu wakuyumbishe kutaka uwe chini yao kwa imani kwamba wewe huwezi kufanya chochote pasipo wao. Uwe na nidhamu binafsi vile unavyotumia muda wako katika kufanikisha mambo yako binafsi na mambo yasiyokusaidia. Muda wako ni maisha yako , ukipoteza muda kwa mambo yasiyo na maana hayo ni maisha yako unachezea. Tunza muda wako kwani ndiyo maisha yako.Muda wa kuishi kwako hapa duniani hakuhusiani na marafiki,ndugu na jamaa, hivyo ukiuchezea muda wako na wao au vitu visivyo na maana muda wako ukiisha , umeisha hakuna atakayekusaidia kuuongeza.
Kumbuka hii.
Aliyekupa muda huo ni Mungu naye akiona huutumii vizuri atakunyang’anya , usisahau kwamba waweza kudanganya tu watu ila siyo Mungu
#Getinspired #Iposiku

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.